Ushauri: Idadi ya Wabunge ipungue ili kupunguza gharama za mishahara na kuwahudumia

so tuwaongeze ili na ss tuongezeke? Lzm unatania.
Idadi ya wananchi ikiongezeka na majimbo yataongezeka itapelekea wabunge kuongezeka....ili kuwaongeza lazima kwanza tuongezeke 🐒
 
Hatuhitaji bunge kuba kiasi hicho. hatuhitaji bunge lenye vigezo vya chini vya elimu na uelewa maana ni watunga sheria na wasimamizi wa dola.
Tutaanza kubadilika kama bunge litabadilika
 
Naunga mkono hoja kila mkoa tunahitaji mbunge mmoja tuu. Pesa zipelekwe kwenye zahanati, shule na maji.
Badala yake wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wachaguliwe na wanawanchi wenyewe.
Ova.
 
Tuanze kuondoa viti maalum pia tuangalie wingi wa majimbo. Kipindi cha magufuli alikua makini tume ya uchaguzi hawakua wanaongeza majimbo ovyoovyo eti kwa kisingizio cha ongezeko la watu. Wanasiasa wanaloby tu ili kuongeza wabunge kwa faida binafsi. Pia uanzishaji ovyo wa maeneo ya utawala usiokua na tija unaishia kuongeza matumizi ya serikali. Watu wanaloby ili kupata vyeo tu.
Badala ya viti maalum vyama vya siasa viwekewe sheria kuhusu wagombea ili kuwepo uwiano wa kijinsia kwa msingi wa weledi wa mtu.
 
Kuna wabunge ni vilaza hata hawakustaili kuwa bungen,wanaongeza matumizi yasiyokuwa na tija.kama abood wa morogoro ni mzigo kwa taifa letu
 
At the same time bado tunataka Chato iwe mkoa hapo itatoa majimbo mapya na gharama inaongezeka kuanzia hao wabunge, wakuu wa Halmashauri, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa plus administrative machinery mpya ambayo inaongeza gharama kibao.

So tujiandae tu kupigwa tozo zaidi.
 
Tupe ufafanunuzi zaidi
Bunge la sasa linawabunge wangapi?
Hii nchi inamajimbo mangapi?
Wapunguzwe wabaki wangapi?
Nchi inawatu wangapi?
Uwiano wa uwakilishi kwa kila mwananchi na mbunge iko vipi?.

Then shauri wabunge kupungua au kuongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…