KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Salamu
Rais wa JMT, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Wazir wa Fedha, Dkt.Mwigulu Nchemba
Ninayo furaha sana kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na huruma kwa baraka zake kuu tunazoendelea kuzishuhudia katika Taifa letu. Kwa namna ya pekee kabisa ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa amani, umoja na mshikamano tulionao kama Taifa.
Rais, pamoja na mambo mengine, ninayo furaha kubwa kukupongeza kwa uongozi wenye matokeo chanya kwa maendeleo yetu kwa kizazi cha sasa na vijavyo, kwa hakika nikiri kusema kwamba ni Uongozi wenye kuacha alama ya matumaini.
Rais, wenye kuitambua dhamira yako njema kwa Taifa letu hatuchoki kukuombea, kukutia moyo na kutumia nafasi na majukwaa mbalimbali kusaidia na kutoa mchango wa Ushauri, Maoni na Mapendekezo ambayo tunaamini yatasaidia kuchochea kusukuma gurudumu la maendeleo yetu mbele.
Rais, nikiwa kama mtanzania ambaye nina tamaa ya kuona mabadiliko chanya kwenye kila eneo, ninawiwa kutoa mchango wa mawazo ambayo yataleta tija kwenye maeneo husika na leo ninawiwa kutoa mchango wangu juu ya wazo la kuigawanya MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA).
Rais, ushauri wangu wa kuigawanya TRA ili zipatikane Mamlaka mbili ambazo tuziite Mamlaka ya Mapato ya Ndani na Mamlaka ya Mapato ya nje linachagizwa pakubwa na upotovu wa Mapato na hilo pengine ni kutokana na ukubwa wa TRA ulionao sasa
Rais, kuigawanya TRA kutasaidia kuleta ufanisi mkubwa katika ukusanyaji mapato katika vyanzo mbalimbali vilivyopo na pia kutasiadia kila Mamlaka kuja na ubunifu wa kivyake ili kuongeza wigo wa kodi kuliko ilivyo sasa.
Rais, katika wazo hili la kuigawanya TRA, Mamlaka ya Mapato ya Ndani ihusike na mapato yote ambayo chanzo cha mapato kiwe ni Tanzania kwa maana ya kwamba kama ni bidhaa iwe imetengezwa Tanzania na Mamlaka ya Mapato ya nje ihusike na mapato yote ambayo Chanzo Chake ni nje ya nchi na bidhaa zote ambazo zimeingizwa kutoka nje ya nchi
Huu ndio Mchango wangu maoni katika suala hili Mhe.Rais, ni matumaini yangu yataleta tija katika ukusanyaji mkubwa wa mapato ya Serikali na kudhibiti upotevu wa mapato kutokana na sababu mbalimbali.
"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"