Ushauri: Inasemekana mpenzi wangu alishawahi kuwa na mahusiano na ndugu zangu!

Ushauri: Inasemekana mpenzi wangu alishawahi kuwa na mahusiano na ndugu zangu!

amilyroley

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
621
Reaction score
1,200
Na-Paste Text yake...

Naombeni msaada wa ushauri ndugu zangu.

Mimi ni msichana na Nina mpenzi wangu tumedumu kwa miaka mitatu sasa. Nilifahamiana naye nikiwa form six na kuanzia wakati huo tukawa wapenzi. Ananipenda sana kuanzia mwanzo had sasa, sijawahi kumkuta hata na text ya binti yeyote kwenye simu yake na sijawah kugombana na boyfriend wangu Huyu kwa ajili ya mwanamke mwingine.

Anajiheshimu na kuniheshumu sana. Zaidi ananihudumia tangu nikiwa kidato cha sita mpaka muda huu nipo mwaka wa pili chuo kikuu hapa mjini.

Anafanya kazi katika kampuni moja ya mawasiliano. Kuanzia nilipokuwa kidato cha sita alinipa chochote nachotaka mpaka muda huu hajawah kubadilika. Kwa asilimia zote yeye ndiye aliyeshugulika michakato yote nilipomaliza kidato cha sita hapa namaanisha fomu za bodi ya mkopp, TCU, jeshi na nyinginezo ni yeye ndiye aliyenijazia kwa pesa zake na kuzituma.

Amehakikisha hadi nafika chuo na mpaka muda huu bado ananihudumia. Napata huduma zote kama mwanamke na shopping ni kila wikiend.

TATIZO LIMEIBUKA.

Zimeibuka taarifa kuwa mpenzi wangu huyu ambaye nampenda sana na tunatarajia kuoana baadaye kuwa kabla hajawa na mimi alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na ndugu zangu wawili, mmoja dada yangu mtoto wa mama mkubwa na mwingine mdogo wangu mtoto wa shangazi.

Inasemekana boy wangu huyu aliwapitia kwa nyakati tofauti kabla hajakutana na mimi lakini. Kati ya hao ndugu zangu mmoja amekubali na kukiri kuwa alitoka naye, ila mwingine amekataa hajatoka na boy wangu.

Na huyu boyfriend wangu amekataa kabisa kuwa hajawah kutoka na ndugu yangu yeyote. Inshu imejulikana tayari katika familia yangu. Kwa tukio hilo mama na kaka zangu wamemkataa kabisa boyfriend wangu kuwa ni laana na hawapo tayari kumuona akija nyumbani baadae kuniposa eti kwa sababu ya tukio hilo kuwa zamani kabla yangu alitoka na ndugu zangu wawili kitu ambacho boyfriend wangu amekataa kabisa kuwa hajawahi na mmoja wa hao dada zangu amekubali alitoka naye ila mwingine amekanusha.

Nampenda sana boyfriend wangu ananipenda sana pia na kunihudumia kwa kila kitu. Nipo njia panda. Ni kweli mapenzi wakat mwingine huhitaji ushauri ni kuamua you kulingana na matakwa ya moyo ila kwa kuwa yamehisisha na familia ndio maana nataka ushauri wenu ndugu zangu.

Nishauri lolote unalohisi ni busara. Nahitaji ushauri wako unisaidie kufanya maamizu.

Nifanyeje Jamani nipo kwenye wakati mgumu sana. Boyfriend wangu huyu anasubiri maamuzi yangu na msimamo wake ni ule ule kuwa hajawahi kutoka na hao ndugu zangu.

NISAIDIENI USHAURI NDUGU ZANGU.
 
Aliyesema mapenzi upofu hakukosea aiseee, mi nimekosa cha kukushauri sababu ya hapa:
".... alitoka na ndugu zangu wawili kitu ambacho boyfriend wangu amekataa kabisa kuwa hajawahi na mmoja wa hao dada zangu amekubali alitoka naye ila mwingine amekanusha. Nampenda sana boyfriend wangu ananipenda sana pia na kunihudumia kwa kila kitu."
 
Mapenzi hayanaga ushauri ni kuamua tu mwenyewe ufanyaje
 
Anakataa kwa sababu hataki kukukosa, kama siku zote hizo yuko na ww na anakuhudumia basi anakupenda,ko ni ww kuamua ata wazaz wako wataheshimu upendo wako,vinginevyo wanadhan anakupitia na kukuacha
 
Kuna mambo kadhaa ya kujiuliza hapa
1. Hizo taarifa zimeanzia wapi, na kwa nia ipi?
2. Zimefikaje nyumbani?
3. Jamaa amekanusha, na dada mmoja kakanusha pia. Mmoja ndiyo kakubali.

Ukute huyo aliyekubali "alipitiwa" ana agenda yake. Na kwanza inakuwaje mwanamke anakubali kuwa "alipitiwa"? Some smell fishy here.

Au labda Jamaa alifanya kweli, but what's the fuss anyway?? Si ilikuwa zamani.

images
 
Kuna mambo kadhaa ya kujiuliza hapa
1. Hizo taarifa zimeanzia wapi, na kwa nia ipi?
2. Zimefikaje nyumbani?
3. Jamaa amekanusha, na dada mmoja kakanusha pia. Mmoja ndiyo kakubali.

Ukute huyo aliyekubali "alipitiwa" ana agenda yake. Na kwanza inakuwaje mwanamke anakubali kuwa "alipitiwa"? Some smell fishy here.

Au labda Jamaa alifanya kweli, but what's the fuss anyway?? Si ilikuwa zamani.

images

Umefanya analysis nzuri kaka angu. So nifanyeje?
 
If n kabla ya yalishapita hayo sumtimes ndugu hatupendani
 
Maamuz ni yako ndugu inategemea hilo jambo umelichukulia uzito kiasi gan jambo lililokwisha pita lisikuharibie mipango yako na ndoto zako usikurupuke cha msingi hakikishamaelewano yana rejea baina ya familia yako na huyo boy wako na heshima inakuwepo kati ya hao ndugu na mwenza wako
 
Umefanya analysis nzuri kaka angu. So nifanyeje?

Ukishikwa shikamana. nazijua ndoa zenye mtu nadogo wake tumbo moja. mbona hao dada zako hawakulalamka wakati wakipinduana. wa mwisho ndiye mshndi.
 
Du, bado watu wanasomesha wachumba tu. Wanaume mbona hamjifunzi tu?? Kimsingi naona umeshaanza figisu za kumpiga jamaa chini hasa baada ya kukusomesha mpaka chuo. All the best but I pity him maana kama yuko humu ataleta mrejesho soon.
 
Naomba nikuulize, hivi na wewe ashakukula au bado
 
Duh! Sasa kama home kwenu wameshamkataa hata tukikushauri itakuwa ni kazi bure tu... Kubali kuwa mkataba wa pango umekwisha hata kama una kodi ya kuendeea kupanga hapo ulipo sio pako. Katafute nyumba ingine.
 
Ulichikigundua ni kwamba ndugu zako si wife material kwa jamaa, we ndio unafaaa. Kama unatafuta malaika keep on looking!
 
Anaekupenda atafanya lolote ata kudanganya ilimradi asipoteze mapenz yako kwake
 
Pole sana kwa kupitia kipindi hiki kigumu. Mungu ni mwema na hakika atakupigania. Wakati mwingine suala la umasikini kwetu sisi waafrika huchangiwa na kutofikiri kwa mantiki.

Mimi nakushauri usonge mbele na "boyfriend" wako na Mungu akipenda mje kuwa mwili mmoja. Masuala ya laana naona usiyazingatie. Katika mila na desturi zetu waafrika tuna "get valve". Kama ni kuepuka laana tambiko au utaratibu wa kimila ufanyike ili kuzuia laana.
Mchunguze vizuri "boyfriend" wako kwani huenda kuna tabia anazo haziwafurahishi nduguzo. Suala ulilosema linatumika kuwatenganisha.

Sisi ni Binadamu, wachunguze nduguzo huenda wana wivu na husda juu ya mahusiano yako. Siunajua ktk jamii suala la kuolewa wengine huchukulia kama ajira.
 
Hata kama amefanya hicho kitu ni huko nyuma, chagua kusamehe msonge mbele. .
You r the one getting married to him sio kaka zako na wazee wako
 
Ina maana wee unawapinga wahenga na ule msemo wao wa KIZURI KULA NA NDUNGUYO?
 
Back
Top Bottom