Ushauri: Jaji Warioba fupisha mchakato wa Katiba!

Ushauri: Jaji Warioba fupisha mchakato wa Katiba!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Tume ya Uundwaji wa Katiba mpya nchini Tanzania inayoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba imeshatoa Rasimu ya Katiba mpya.Ni Rasimu ya Kwanza. Bado Rasimu mbili.Moja itajadiliwa na kuidhinishwa na Bunge la Katiba (ambapo Rais atalibadili Bunge la Muungano hili la sasa kuwa Bunge la Katiba). Na Rasimu ya mwisho itapigiwa kura ya 'ndiyo' au 'hapana' na wananchi wote wenye umri wa kupiga kura. Hivi sasa Rasimu ya kwanza inajadiliwa na Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Kimsingi,Mabaraza haya ya Katiba yanamilikiwa na CCM.Ndiyo kusema,asilimia zaidi ya 80 ya Wajumbe wa Mabaraza hayo ni wa CCM. CCM huko Mabarazani wana nguvu ya kusema na kupitisha chochote. Na katika kuwasaidia wajumbe wetu wa CCM kwenye Mabaraza hayo,CCM imetoa waraka unaoainisha mambo ya kuyasema (tena kama yalivyoandikwa) katika Waraka huo wa CCM. Ni wazi kuwa majadiliano yote ya Mabaraza ya Katiba yataishia kwa ushindi wa CCM kihoja na kihaja kutokana na wingi uliopo. Namshauri Jaji Warioba na Tume yake kufupisha mchakato huo.

Ni kuchukua Waraka wa CCM na kutoa Rasimu ya pili. Hii ni kwakuwa, Wajumbe wote wa CCM,ambao ndio wengi Mabarazani, wanausoma au kuusema Waraka wa Chama tu.Hawana jipya. Hawana mawazo yao huru. Wanatupotezea muda na kutuchezea akili zetu tu. Ni maigizo tu.Basi. Rasimu ya pili itolewe na ijadiliwe na Bunge la Katiba. Napo,mambo yatakuwa kama kwenye Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Pia hapo,msimamo wa mwisho utajulikana mapema kutokana na wingi wa Wabunge wa CCM Bungeni humo.

Tutauponya muda pia. Haraka sana tutaingia kwenye kura za maoni. Hatimaye tutapata au kukosa Katiba mpya. Jaji Warioba anapaswa kufupisha mchakato huu wa Katiba ya Muungano kwakuwa tutahitaji muda nasi watanganyika kuunda Katiba yetu. Na Wazanzibari vivyohivyo. Tuna muda mfupi kuliko urefu usio na msingi wa mchakato wa Katiba zote tatu. Watanzania tunataka tuchaguane kwa Katiba mpya hapo 2015.Tunataka kuona Katiba mpya hizi zinakuwa kweli. Tume na mnisikie!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.­­
 
CCM imetengeza misukule mingi sana hapa nchini. Uzuri ni kuwa sheitwan hata angejitahidi vipi hawezi kumshinda Mungu muumba wa mbingu na nchi. CCM ni CHAMA CHA MASHEITWAN
 
Mzee Tupatupa unasemaje mnataka kuunda katiba yenu ya Tanganyika wakati umeshakiri kuwa CCM imeshaipiku rasimu ya kwanza na ijayo itakuwa sawasawa na kama CCM inavyotaka, yaani serikali mbili?
 
Warioba alikosea mno kuipa ishu ya Tanganyika kuwa the ndo muhimu zaidi
sasa haya ya muhimu kama Tume huru ya uchaguzi
na kudhibiti madaraka ya Rais hayajadiliwi
 
Back
Top Bottom