Ushauri Jamani on App Marketing [emoji120]

Brave_Idiot

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2023
Posts
209
Reaction score
368
Mzee wangu anaamini sana kwenye kilimo, nahofia nikimuomba mtaji wakuipromote app yangu ataona huyu kijana ananiletea utandawazi nyumbani kwangu. Ninamsimamia kazi yake moja huku Dar, yeye yupo Mwanza. Sasa nataka nivute laki tano chapu kwenye mfuko wa mauzo yake, niipromote hii app na ndani ya wiki niwe nauwezo wakuilejesha hela yake kabla hajanishtukia. Naamini nikiweza Kutengeneza downloads laki moja playstore, haitokua ngumu kurudisha hicho kiasi au na zaidi.

App inamfumo kama wa YouTube 100%, sasa nilikua naomba ushauri wa mfumo gani nitumie kuipromote kwa haraka nakufikia hayo malengo. Kiupande wangu nilikua nafikilia kuwatumia ma tiktoker kama clam vevo au Steve mweusi sema naona Balance ndo inakataa!!!

Msaada wa ushauri jamani nisije fukuzwa nyumbani [emoji26][emoji23]
 
Ongea na mzee kwanza coz hicho unachotaka kufanya huna uhakika nacho asilimia 100 kuna kubugi ukaharibu kote huko kweny app na kwa mzee jarbu kuzungumza nae kwa uzuri kwanza.
 
Kama ni una tafuta traffic ya bongo umefel tayari. Ungetengeneza app ya status saver then uka tafuta traffic SA/Brazil hiyo 500k kwa wiki inarudi chapu tu.
Sasa status saver naingizaje pey
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…