Viuatilifu ni kemikali za asili au za kisasa zinazotumiwa na wakulima ili kupambana zidi ya wadudu waharibifu na magonjwa mbali mbali yanaoshambulia mazao yao yawapo shambani au yakiwa ghalani.
Imezoeleka wakulima wengi hutumia mbolea za viwandani ili kuipatia mimea virutubisho muhimu kwa ajili ya ukuaji hivyo kuleta mazao mengi kwa eneo husika, wakati huo huo matumizi ya viuatilifu ili kupambana na wadudu na magonjwa nyemelezi katika mazao pamoja na bidhaa za mazao zilizohifadhiwa stoo (kwenye maghala).
Tukiangalia kwenye viuatilifu, kila kiuatilifu kina muda wake maalumu ambao kinatakiwa kikae shambani au juu ya zao husika toka siku ya kuwekwa au kupuliziwa shambani mpaka siku zao husika litakapovunwa tayari kwa matumizi ya binadamu bila kumdhuru mtumiaji.
Kwa mfano kiuatilifu X kinatakiwa kiachwe kwa muda wa siku 30 toka siku ya kupuliziwa shambani mpaka siku ya kuvuna zao hilo. Siku hizo 30 ni idadi ya siku ambazo sumu iliyopo katika kiuatilifu X itapoteza nguvu hivyo kutomdhuru mtumiaji au mlaji wa zao husika. Hivyo endapo zao hilo litaliwa kabla ya siku hizo 30 basi kuna uwezekano mkubwa kwa mlaji kuathiriwa na sumu hiyo hivyo kupata magonjwa kama saratani ya utumbo.
Wakulima wengi hasa wa mboga mboga maeneo ya mjini wamekua hawafuati utaratibu huo wa kuacha mazao kwa kipindi kinachoshauriwa kipite kabla ya kuvuna zao hilo hivyo kuziweka hatarini afya za walaji.
Kipi kinachofanywa na wakulima wa mboga mboga hasa maeneo ya mjini.
Wakulima wengi wa mboga hawajui mda sahihi wa kupiga dawa katika mazao yao ili kupambana na wadudu waharibifu pamoja na magonjwa. Unakuta mtu anapiga dawa wakati nyanya tayari ishabadirika ile rangi ya ganda lake na baada ya siki tatu (3) anavuna ni lazima mtumiaji aathiriwe na keemikali hizo.
A. Kipi kitatokea endapo mtu atakula zao lenye mrundikano wa sumu zilizopo katika viuatilifu.
1. Madhara ya mrundikano wa sumu hizo huwa hayaonekani kwa wakati huo huo bali ni matokeo ya kurudia mara kwa mara kula sumu hiyo hivyo kujengeka kwa saratani ya tumbo. Unaweza kula leo lakini madhara yake yakaonekana miaka 15 baadae hivyo tunatakiwa kuwa makini sana na kemikali hizo.
2. Uchafuzi wa mazingira kutokana na maji tunayomwaga baada ya kuosha mboga mboga zenye sumu na endapo yatafika kwenye vyanzo vya maji basi tutakua tupo hatarini kuugua endapo yatatumika kama maji ya kunywa.
B. Ni kipi kifanyike kwa upande wa serikali ili kuepusha madhara yatokanayo na uzembe huu.
1. Kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu ili wajue mda upi sahihi kupiga dawa flani katika zao flani na katika kiwango kinachotakiwa ili kuhakikisha sumu itakayotumika inaisha kabla ya kuvuna au kupeleka zao sokoni.
2. Elimu itolewe kwa wakulima juu ya mbinu mbadala za kupambana na magonjwa pamoja na wadudu waharibifu mfano; kilimo mseto na kilimo cha mzunguko msimu hadi msimu.
3. Serikali ikishirikiana na wadau wa sekta za kilimo na afya iweke utaratibu maalumu wa kupima kiwango cha sumu kilichobaki (Resdual amount) katika bidhaa za kilimo kabla ya kuruhusu kuingizwa sokoni kwa matumizi ya binadamu.
4. Serikali ikishirikiana na wadau wa kilimo tuhamasishe angalau kuwa na bustani ndogo ndogo za mboga katika miji zetu tunazoweza lima kwa kutumia viuatilifu vya kienyeji.
5. Kuhamasisha wakulima kufanya kilimo hai au kutumia viuatilifu asili kama vile vimiminika vitokanavyo na mbegu, majani au mizizi ya Mlonge, mwarobaini, Tangawizi pamoja na pilipili.
C. Kipi ufanye ili kuepuka kununua mboga mboga za majani zenye kiwango kingi cha sumu.
1. Epuka kabisa kununua mboga mboga ambazo hazina hata dalili kidogo zinazoonesha kushambuliwa na wadudu waharibifu, mfano; chagua chainizi inayoonesha kuwa imeliwa na wadudu kuliko ambayo haijaliwa.
2. Kuosha kwa umakini mboga mboga na viungo vingine kabla ya kuvitumia japo kuna baadhi ya mboga hupoteza virutubisho kwa kuoshwa sana.
3. Kujiwekea utaratibu wa kuwa na bustan ndogo ndogo za mboga mboga zinazoweza limwa hata wima kwa wale wenye maeneo madogo.
Lakini pia kwa upande wa sumu kuvu au kiuatilifu kinachotumika kuhifadhia nafaka hasa mahindi na maharage, sumu hii pia ina mda wake maalumu inatakiwa ikae stoo kabla ya nafaka kuuzwa au kusagwa tayari kwa matumizi ya binadamu.
Kipi kinachofanywa na wauzaji wengi wa nafaka na vyakula vitokanavyo na nafaka.
Wauzaji wengi hawazingatii mda sahihi wa kuiacha dawa ipoteze makali kabla ya kupeleka sokoni nafaka husika ambao huwa ni angalau miezi mitatu mpaka sita kwa baadhi ya sumu.
Wauzaji wa unga hasa Donna huwa hawaoshi mahindi yao kabla ya kusaga hivyo moja kwa moja kuweka hatarini afya za wateja wao kutokana na madhara yatokanayo na mrundikano wa sumu kuvu mwilini mwao.
Kipi kifanyike kuepukana na madhara ya sumu itumikayo kuhifadhi nafaka.
Serikali iweke utaratibu wa kupima kiwango cha mabaki ya sumu katika kila mizigo ya nafaka inayoingia sokoni ili kuwaepusha watumiaji.
Tuweke utaratibu wa kujitengenezea unga wetu wenyewe hasa walaji wa donna kwa kununua mahindi na kisha kuyaosha na kuyaacha yakauke vizuri kabla ya kusaga.
Tuepuke kununua mahindi ya mbegu kwa ajiri ya matumizi ya chakula majumbani mwetu. (Kuna viashiria hutumika kutofautisha mahindi kwa ajili ya chakula na mahindi kwa ajili ya mbegu).
Wizara ya kilimo , Wizara ya afya kwa kushirikiana na jamii tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kulinda kizazi chetu kilichopo na kijacho dhidi ya magonjwa mbali mbali yasiyoambukizwa sababu madhara ya kemikali hizi huwa hayaonekani ghafla bali hujijenga siku mpaka siku na kuwa sugu.
Ahsanteni.

Upvote
6