Ushauri; jinsi ya kuanzisha coffee shop.

Ushauri; jinsi ya kuanzisha coffee shop.

LIBRARY

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2012
Posts
231
Reaction score
238
Habari zenu wakuu,
baada ya mafanikio na ushirikiano mkubwa mliounyesha hapa jamvini juu ya kijana wenu, Leo ningependa kuja na swala jingine kidogo ambalo nataka niwashirikishe. Naitaji ushauri wenu juu ya biashara flani ya outdoor coffee shop. Kwa sasa nimeshapata kiosk. So ningependa kupata ushauri wenu katika biashara hii au juu ya mambo yafuatayo;
1. Cheap commercial coffee machines
2. Commercial display frigerator
3. n.k
karibuni.
 
1- Tembelea katika viosk ama sehemu zingine amabazo wanatoa huduma kama yako, omba kuonana na wamiliki then waulize wao wamenunua wapi vifaa vyao na kwa kiasi gani? Pia waulize baadhi ya mambo yanayohusiana na biashara hiyo ambayo unapaswa kujua na kujifunza.
2 - Nenda posta na Kariakoo kama upo Dar Es Salaam kuna sehemu nyingi wanauza vifaa aina hiyo pamoja na vile vya mahotelini na migahawa. Kila la kheri.
 
Umefanya research na soko lipo mkuu ?
Wanywaji wa Coffee kwa bongo ni wengi ?
Je joto halitakuharibia biashara yako ?

Nadhani sababu ya market kuwa narrow ni vema kutokuji-limit na coffee pekee bali weka mgahawa ambao una refreshments tofauti tofauti ili uweze kupata watu tofauti, kama location ni nzuri na menu ni nzuri watu watakuja (weka soft drinks na snacks za kutosha as well as hot drinks)

Mambo ya Starbucks nadhani kwa bongo sio kwa sana ndio maana hata huko ughaibuni chips mayai sio kwa sana (inategemea nature na culture ya watu)

th
 
Pale Moshi Chama cha Ushirika(KNCU) wameanzisha yao na inafanya vizuri sana ingawa wateja wakuu ni watu wa nchi za Ulaya. Ingawa investment yake ni kubwa haswa upate watu ambao wako competent kuandaa kahawa ya quality ya hali ya juu, if possible wapeleke wakajifunze nje ambako wa utamaduni huu wa coffee bar. Jitahidi ufanye kitu cha tofauti ili u-convice hata wazawa waikubali hii huduma, ingawa hatuna mazoea hayo. Kwa ushauri wangu anza sehemu kama Arusha ukilenga watalii na pia kwa sababu ya hali ya hewa.
 
ahsante sana mkuu Sun Wu,
coffee shop itakua maeneo ya barabara ya sokoine drive, Barbara ile inatumiwa na sana na wapita njia Hasa mida ya hasubuh wakati wa kwenda kazini pamoja na wakati wa kurudi. Patakua na bidhaa tofautitofaut na refreshments zingine ndio maana nimeulizia pamoja na displaying fregirator. bites zitakuepo bila kusahau snacks mbalimbali. coffee shop ni line of business ambayo itaipa title hako ka mgahawa kangu. Kuhusu maswala ya hali ya hewa (joto) mgahawa utakua ni outdoor, na iced tea au barafu zilizochanganywa kwenye coffee Nazo zitapatikana. Kuhusu wateja, biashara hii nimeiona sana kwenye migahawa mikubwa huku gharama zake nazo zikiwa juu kwa mfano pale golden 2lip restaurant 1cup of espresso ni 5000tsh. Kwa mmi nitawelenga wananchi wenzangu wa hali ya chini hata 1000 Tu na kama utahitaji mbwembwe inaweza ikaongezeka kidogo.
Karibu.
 
1- Tembelea katika viosk ama sehemu zingine amabazo wanatoa huduma kama yako, omba kuonana na wamiliki then waulize wao wamenunua wapi vifaa vyao na kwa kiasi gani? Pia waulize baadhi ya mambo yanayohusiana na biashara hiyo ambayo unapaswa kujua na kujifunza.
2 - Nenda posta na Kariakoo kama upo Dar Es Salaam kuna sehemu nyingi wanauza vifaa aina hiyo pamoja na vile vya mahotelini na migahawa. Kila la kheri.

mkuu hadi sasa sijapata kufahamu kama kuna local coffee shops kwani kwenye haya ma-mgahawa makubwa owners wake hadi uje uonane nao ni shughuli kidogo.
Ahsante
 
mkuu hadi sasa sijapata kufahamu kama kuna local coffee shops kwani kwenye haya ma-mgahawa makubwa owners wake hadi uje uonane nao ni shughuli kidogo.
Ahsante

Haina haja ya kumsumbua owner, wapishi na wahudumu wanaelewa vizuri sana na watakuwa wawazi tu kwake akiwa friendly! Good move brother LIBRARY
 
Last edited by a moderator:
Pale Moshi Chama cha Ushirika(KNCU) wameanzisha yao na inafanya vizuri sana ingawa wateja wakuu ni watu wa nchi za Ulaya. Ingawa investment yake ni kubwa haswa upate watu ambao wako competent kuandaa kahawa ya quality ya hali ya juu, if possible wapeleke wakajifunze nje ambako wa utamaduni huu wa coffee bar. Jitahidi ufanye kitu cha tofauti ili u-convice hata wazawa waikubali hii huduma, ingawa hatuna mazoea hayo. Kwa ushauri wangu anza sehemu kama Arusha ukilenga watalii na pia kwa sababu ya hali ya hewa.

ahsante kwa ushauri mkuu,
Mtaji wangu sio mkubwa kiivyo I mean siwezi vuka mipaka ya DSM kwa sasa. Mtaalamu mmoja wa kutengeneza mambo hayo ninaye alikua akifanya kazi sehemu moja ila kwa sasa Yuko nyumbani na maelekezo mengine nadhani mtandao utatusaidi isitoshe mmi mwenyewe ni library.
 
Haina haja ya kumsumbua owner, wapishi na wahudumu wanaelewa vizuri sana na watakuwa wawazi tu kwake akiwa friendly! Good move brother LIBRARY
ahsante mkuu.
 
Last edited by a moderator:
kama upo dar mkuu nenda pale mapipa kuna ile internet cafe kale kagorofa pale uliza mmiliki wake alikua baharia na alikua analeta vitu vya migahawa safi kabisa hasa hayo mafridge mwambie magembe kakuelekeza wa tipha hotel tabora
 
Back
Top Bottom