SoC02 Ushauri jinsi ya kuboresha Elimu nchini

SoC02 Ushauri jinsi ya kuboresha Elimu nchini

Stories of Change - 2022 Competition

Manvolvo

New Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
1
Reaction score
0
ANDIKO LANGU KUHUSU ELIMU

Elimu ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.

Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, kuhesabu Mitaala yote ipitiwe upya kwa masomo yote tuachane na ukoloni tuwe wa kisasa zaidi na Serikali iajiri walimu wachache wenye uwezo na bidii na sio somo moja shule moja walimu 15/zaidi. Elimu isiwe bure ili kupeleka wazazi na wanafunzi kuithamini elimu kwamaana cha bure hakithaminiwi kama kitu ulichokitafuta kwa shida au taabu.

Uwepo wa wastani wakupanda daraja kwa kila kidato/darasa kama mwenzetu wa shule binafsi wanavyofanya. Nakingereza kitumike toka shule za msingi mpaka mwisho

Serikali na taasisi binafsi ziboreshe maslahi na mazingira ya kazi ya walimu kazini hadi wanakoishi. Pia shule ziwe na maktaba zenye vitabu vya kutosha ili kurudisha utamaduni wakujisomea uliotoweka kutoka na utandawazi. Kozi na semina za elimu mara kwa mara zinahitajika ili waendane na mabadiliko.

Ukaguzi mashuleni mwetu nimuhimu sana pia kuwepo na sheria kali na adhabu kali kwa walimu wazembe. Lakini walimu wape posho na na vitendea kazi vilivyo kamilika./ Stahiki za walimu na posho ziongezwe ikiwezekana walipwe kutokana na mazingira wanayoishi au mazingira wanayofanyia kazi.

ANGALIZO: Elimu ndio inabaki baada ya mtu kusahau kile mtu amejifunza shuleni na siyo masomo yaliyofundishwa darasani

Nampongeza Mh: Profesa Adolf Mkenda kwa utendaji kazi wake

Asante: Kwa uongozi wote na wa tendakazi wa JAMIIFORUMS

Nawasilisha andiko-; EMULISON BYANGARATFE.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom