USHAURI: Jinsi ya kuepuka kununua nyumba, kiwanja penye mgogoro

USHAURI: Jinsi ya kuepuka kununua nyumba, kiwanja penye mgogoro

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
KATIKA makala zilizopita nilieleza mambo muhimu yanayopaswa kuwepo kwenye mkataba pindi mtu anapotaka kununua nyumba au kiwanja. Nilisema mkataba lazima uonyeshe ni jinsi gani mgogoro utakavyotatuliwa pindi utakapotokea baina ya wahusika wa mkataba huo.


Nilisema mkataba lazima ueleze kwamba pindi mgogoro utakapotokea, basi muuzaji atawajibika katika kuhakikisha anatoa ushirikiano kwa mnunuzi kwa lengo la kumaliza mgogoro huo, na pia kwamba muuzaji, kama ana mke, basi mke huyo lazima aandaliwe waraka unaoitwa Ridhaa ya Mwanandoa, ambao ni tofauti na mkataba. Mke huyo anatakiwa asaini waraka huo pamoja na kuweka picha yake.


Kwa wale ambao hawakubahatika kusoma makala zangu hizo zilizopita juu ya mada hizo za kisheria kuhusu ununuzi na uuzaji kupitia FikraPevu, basi wanaweza wakazi-goole kwa kuandika Makala Sheria, watazipata na kuzisoma. Katika mada ya leo tutajadili hatua muhimu ambazo mnunuzi wa kiwanja au nyumba anapaswa kuzifuata kabla ya kufanya mwamala wowote wa manunuzi.

Moja ya hatua hiyo muhimu kabla ya kufanya chochote, kitaalamu inaitwa ‘Official Search'. Kwa lugha rahisi, hatua hiyo yaweza kuitwa utafiti, upekuzi, upelelezi au upembuzi rasmi ambao hufanywa na wanasheria. Kwa kadri ya makala haya, napendekeza tutumie neno upelelezi.

Soma zaidi makala hii: http://www.fikrapevu.com/jinsi-ya-kuepuka-kununua-nyumba-kiwanja-penye-mgogoro/

 
Back
Top Bottom