Ushauri juu kesi hii je nitaishinda.

Mbona maelezo yako yanaonesha kama wewe ndo muhusika mwenyewe. Ningekuwa ndo hakimu na umeeleza hivyo ningekulima miaka yako 5 safi kabisa
 
Daa kama hukuiba alafu huna maswali yakumnyoosha basi unatakiwa kunyooka mwenyewe
 
Kipindi amelala aliskia watu wanagusa kitasa cha mlango wake.
Mara akaskia kama upepo unapuliza na dirisha kufunguka (dirisha ni la nyavu na nondo linafungiwa ndani) basi ndipo alipoona watu wakichukua simu na baadae wakibeba na computer mezani
umehusika lipa mali za watu, wizi sio mzuri
 
Muulize maswali yanayohusu umbali na pia kiasi cha mwanga unaoruhusu kuona na kutambua.Nenda mahakamani na gazeti kaa umbali wa hatua tatu umwambie akusomee,akishindwa kusoma mtwange swali kuwa kama umeshindwa kutambua maandishi yaliyopo hatua tatu toka ulipo na kuyasoma uliwezaje kutambua sura yangu umbali mrefu na unaonekana una matatizo ya macho.Muulize technical questins.
 
Hii nmeielewa asee asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…