Ushauri juu ya tatizo la kutowaka kwa gari linapokua limepata moto

Ushauri juu ya tatizo la kutowaka kwa gari linapokua limepata moto

DALOOKER

New Member
Joined
Jan 8, 2017
Posts
4
Reaction score
4
Habari, nina changamoto ya gari (tipa, isuzu, double diff tani 10 , engine dizel ya v10). Gari in inawaka vizuri tu ikiwa imepoa ila ikisha tembea na kupata moto, gari haiwaki inakua nzito kuwaka.

Stata inakua nzito kuzungusha injini, yani ina zungusha injini taratibu mno kama betri hazina chaji vile.

Nimeangalia stata sio shida. Nimekagua waya za kwanda kwenye stata hazina shida umeme unafika vizuri.

Nimekagua betri ziko vizuri
na wakati zina fanya hiyo tabia unakuta betri zina volt 26 zote mbili kwa pamoja.

Na ukiiacha kama lisaa au lisaa na nusu na kuendelea gari inawaka.
Msaada kwa ambae ashakutana na hii changamoto.
 
Mfumo wa kupooza Engen mbovu huo. kagua maji mara kwa mara au peleka kwa fundi.
 
Back
Top Bottom