SoC01 Ushauri juu ya Ulaji bora kwa afya bora

SoC01 Ushauri juu ya Ulaji bora kwa afya bora

Stories of Change - 2021 Competition

Nawatania

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
148
Reaction score
549
ULAJI BORA NI NINI?

Ulaji bora ni aina ya mlo ambao hutokana na kula chakula chenye mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi matano ya chakula.

Mfano Ugali, Samaki,Kisanvu, nanasi na karanga huu ni mfano wa mlo kamili, na unashauliwa kula mlo kamili mara tatu kwa siku.

Makundi yenyewe ya vyakula ni kama ifuatavyo

Kundi la kwanza:

Kundi la kwanza ni vyakula jamii ya Nafaka, mizizi na ndizi, Mfano vyakula vya nafaka ni Mahindi, Ngano, Michele, Ulezi, Mtama na Uwele.

Mizizi ni Viazi vitamu,Viazi mviringo, Magimbi, Viazi vikuu, Mihogo na ndizi.

Kundi la pili:

Kundi la pili ni vyakula jamii Kunde na vyakula asili ya wanyama. Mfano Maharage, kunde, njugu mawe, mbaazi, Njegere, Choroko, karanga na dengu.
Vyakula vya asili ya wanyama ni pamoja na nyama aina zote, samaki, maziwa,Jibini, dagaa,mayai na wadudu wanaoliwa kama kumbikumbi senene na nzige.

Kundi la tatu

Kundi la tatu ni vyakula jamii ya mboga mboga zinazojumuisha majani ya mbogamboga, kunde, matembele, mchicha, sukuma-wiki, spinachi, kisanvu, mlenda, figiri na mnafu.
Nyingine ni karoti, bamia, nyanya, biringanyi, maboga, matango na nyanya chungu.

Kundi la nne

Kundi la nne ni matunda mfano mapera, ubuyu, ukwaju, nanasi, embe, machungwa, mafenesi, mastafeli, machenza, zambarau, matopetope, mapasheni, mapapai na maembe.

Kundi la tano

Kundi la tano ni mafuta na sukari mfano siagi, mafuta ya kupikia, mbegu zinazotoa mafuta kama ufuta, korosho, kweme, karanga na sukari.

Mambo ya kuzingatia:

Unapokula hakikisha unazingatia angalau chakula kimoja kwa siku kutoka katika makundi hayo matano ya vyakula kumbuka ulaji wa mbogamboga na matunda maana usaidia sana kuimalisha mfumo wa kinga ya mwili na kukuepusha na maradhi mbalimbali.

Zingatia pia kutafuna chakula kwa ufasaha mdomoni kabla ya kukimeza ili kusaidia mmeng'enyo wa chakula hicho kuwa rahisi.

Kunywa maji mengi angalau maji Lita moja na nusu kwa siku au glasi nane pia kunywa juisi iliyotengenezwa na matunda mbalimbali na sio juisi ya kiwandani jiwekee utaratibu wa kujitengenezea nyumbani.

Mambo ya kuyaepuka:

Epuka kula sana vyakula vyenye mafuta mengi mfano chipusi, maana usababisha unene kupiga kiasi, kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa sugu kama vile magonjwa ya moyo, kisukari na shinikizo la damu.

Hapa tunashauriwa kupenda kuchoma au kuchemusha vyakula ambavyo kuna uwezekano wa kuvichemsha au kuvichoma kuliko kuvikaanga mfano nyama, ndizi, mihogo, Viazi samaki na vingine.

Epuka pia kula vyakula vyenye chumvi nyingi maana huongeza uwezekano wa kupata shinikizo la damu na baadhi ya aina za saratani.

Hivyo nashauri tujitahidi kufuata miongozo ya ulaji ili kulinda afya zetu.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom