article
Senior Member
- Sep 10, 2016
- 186
- 344
Kampuni ya Vodacom ipo mbioni kuanza kuuza hisa za awali (IPO) kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) zenye samani ya Tshs. 500 billioni mapema mwakani.
Kutokana rekodi ya kibiashara huko nyuma ni wazi kwamba watu wengi watavutiwa na kununua IPO(Initial Public offering) kwa kasi kubwa pale zitakapoanza kuuzwa lakini kama mwekezaji lazima ufahamu yafuatayo ambayo ni muhimu sana kabla haujanunua hisa hizo:
1.Aina ya hisa: zipo haina mbalimbali za hisa na kila moja ikiwa na uzuri na ubaya wake.Nategemea Vodacom watauza mchanganyiko wa "Ordinary shares" na "preference shares". au "ordinary shares" peke yake. Ordinary shares ni nzuri kwa kuwa zinakufanya uwe mmiliki halali wa kinachobakia cha Vodacom baada ya kutoa madeni yake yote pia unakuwa unapata faida isiyo na kikomo pia unakuwa unahusishwa katika maamuzi muhimu ya Kampuni na ubaya wake mkubwa ni kwamba uwezi kupata gawio kama "Preference shareholders" hawajalipwa gawio lao na hasara ya kambuni inapunguzwa kwenye mtaji wako."Preference share" ni nzuri kwa kuwa zinakupa uwakika wa gawio na unakuwa wa kwanza kupata gawio kabla ya "ordinary shareholders" awajapata na hasara ya kampuni inakuwa haikuhusu lakini ubaya wake ni kwamba unakuwa siyo mmiliki wa kampuni bali mtu unayeidai kampuni na unakuwa uwezi kuhusishwa kwenye maamuzi muhimu ya Kampuni.
2.Malengo ya mtaji Mpya: Kabla ujanunua hisa hizi inakupaswa ufahamu eneo la uwekezaji la mtaji mpya na kwa nini imelazimika kuongeza mtaji kwa Vodacom .Hili litakusaidia kuona kama uwekezaji huu utapelekea faida ya Vodacom kuongezeka na wewe kupata faida.
3.Taarifa za fedha na Ripoti za mwaka za Vodacom:unatakiwa ufahamu taarifa muhimu zinazohusiana na faida au hasara,msimamo wa biashara, umumiminikaji wa fedha taslimu na mabadiliko ya mtaji za Vodacom kwa kipindi cha nyuma hii itakuwezesha kujua kama fedha zako umeziweka sehemu salama.Ni vizuri ukawekeza fedha zako huko kama Vodacom inayoonesha historia nzuri ya kutoa gawio (Dividend) kwa wamiliki wa kampuni pia agalia madhara ya "convertible financial instruments e.g convertible corporate bonds,convertible preference shares) kama zipo kwenye pato la kila hisa (EPS) ya Vodacom .Vodacom isiwe na mzigo mkubwa wa madeni pia isiwe imeshitakiwa Mahakamani kwa kosa linalohatarisha uhai wake au litakalopelekea Vodacom kulipa faini kubwa.
4.Wapinzani wa kibiashara na sifa za soko husika : Kabla haujanunua hisa za Vodacom ni vizuri ukatathmini misimamo wa biashara wa wapinzani wake na kama wapinzani wake hawatabadilisha mikakati yao ya kibiashara kutokana na hatua ya Vodacom kuuza IPO pia agalia soko la bidhaa husika kama litabadilika kutokana na Vodacom kuongeza mtaji, angalia asilimia za soko la huduma ya simu ambazo Vodacom inazo kwa sasa na malengo ya eneo la soko baada ya kupata mtaji mpya na kwa nini uongozi wa kampuni unaamini hivyo.
5.Uchumi na Siasa: Kabla haujanunua hisa za Vodacom ni vizuri ukafanya tathmini ya uchumi kwa ujumla kwenye eneo ambalo Vodacom inatoa huduma zake hasa inayohusiana na kipato cha wateja wake,mfumuko wa bei na riba pia ni vizuri ukaangalia kama maamuzi ya kisiasa ya sasa na yanayotegewa katika eneo husika hayawezi kuathiri Biashara ya Vodacom.
Nawasilisha,
Article.