Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Bandugu, mhanga wa utekaji, uteswaji na uuaji Sativa aliyeokotwa huko Katavi amemaliza ugomvi na kufungua sintofahamu kwa nani aliyemteka, kumtesa na kumtupa porini baada ya kumpiga risasi ya kichwa.
Sativa amejitokeza hadharani na kumtaja kuwa Kamanda wa Polisi, ACP Faustine Mafwele wa Osterbay jijini Dar es salaam kwamba ndiye alimteka na kumfunga pingu na kwenda "kumuua" huko Katavi.
Pia soma: Pre GE2025 - Kwanini Polisi haijibu tuhuma alizotoa Sativa juu ya Faustine Mafwele kuhusika kwenye utekaji wake?
Nashauri kwamba ili kuthibitisha maneno ya Sativa basi Afande Mafwele achukue hatua na kumfungulia kesi Sativa ili athibitishe pasi na shaka. Lakini kama Mafwele atakaa kimya basi tutatoa hukumu ya "silence means yes". Sasa kama ni Yes, basi Jeshi la Polisi na Serikali ijihoji ni kwa nini liendelee kuwa na muuaji ndani ya Jeshi hilo? Hii inaweza kuwa ni hatua moja katika kulisafisha jeshi hilo.
Sativa ameenda mbali na kudai bado Mafwele anamtafuta ammalizia maana ana unfinished business. Kwamba kumuua Sativa ndiyo finished business. Kwamba likitokea lolote kwa Sativa basi Mafwele awajibike.
Hii ni hatari mno maana maadui wengine wa Sativa wanaweza kumuua Sativa na Mafwele kuangushiwa jumba bovu. Kama kweli Mafwele anadhani ni msafi basi amfungulie kesi Sativa kwa kumchafua mbele ya umma kuwa ni muuaji. Hii inweza kuleta usumbufu si tu kwa umma lakini ni mke gani anaweza kuishi na miuaji? Ni watoto gani wataishi na baba muuaji? Ni ndugu gani wataishi na muuaji? Ni majirani gani waishi na muuaji? Mafwele atatengwa na kukimbiwa si tu na kila mtu bali hata wanyama wenye kunusa harufu ya kifo kama mbwa watamkimbia Faustine Mafwele.
Ova!