Ushauri kati ya Nissan X-trail Fourth Generation na Subari Foresta Fourth Generation

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Wakuu salama?

Mfano mtu anataka ku experience the difference, ahame kutoka Toyota Rav 4/Harrier/Vanguard. Je kati ya hizi gari mbili ipi nzuri zaidi ama abakie tu kwa Toyota?

Gari hizo ni Foresta Toleo la nne na X-trail toleo la nne.


Ahsante sana
 
Subaru Forester 4th generation unyama sana.
 
Binafsi ntachagua Xtrail yoyote ya kuanzia 2010 na kuendelea. Zile ambazo odometer ipo nyuma ya steering wheel, achana na zile ambazo odo ipo katikati kama ist, mpaka mtu wa siti ya nyuma anaona gari inaenda speed gani.

Imekaa kidingi sana halafu ina space kubwa pale nyuma. Good for family trips na boot iko na nafasi. Mengine sijui maana sijawahi miliki Xtrail. Nissan pekee niliyowahi miliki ni Wingroad na sikuwahi jutia. I just love muonekano ule wa Xtrail.
 
Achukue nissan Xtrail toleo la kwanza ndio tunatumia sisi wagumu a.k.a wakulima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…