Hapo ni Option kubwa sana ndio maana watu hawakupi ushauri vizuri ila wanakupa opinions tu.
Kikubwa cha kwanza tukuulize, unataka gari hasa hasa la nini? Usiseme la kwendea tu huko wapi sijui. Kumbuka kwa mwaka unaweza kua unaenda mara 2 au mara 1, ila muda mwingi utakua unaifanyia misele mingine tu hapo Mwanza. Kwahiyo tunapenda tujue gari ilo utakua unalitumia sana sana kwa nini?
Hafu pili, unataka model gani? Maana umesema tu Subaru yenye engine ya cc1500 na ukasema tu Bima 1 Series.
Mimi nitaongelea kidogo hapa ilo swala la pili.
Kwa kukuona, nadhani taste yako ni Hatchback, coz 1 series ni Hatchback so nadhani ata Subaru utaitaka Hatchback, ambayo nadhani ni Impreza.
ZOte sio mbaya ila zina radha tofauti sana. Mimi nashauri ungeenda kwa Wajerumani, BMW 1 Series, E87 (2004 -2011), hutakaa ukajuta.
BMW cars ni spacious, reliable, comfortable, speed ndio SI unit yake (240kph), barabarani stable, na mbaya zaidi, it is Ultimate Driving Machine. Usiogope kuhusu spare, utazipata nyingi tu Mjini hapa (Noble Motors).
View attachment 472662