Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Nashauri katika kupambana na ugonjwa corona, viongozi wakuu wa kitaifa kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, wawe wanavaa barakoa kila wanapojitokeza hadharani iwe ni katika mikutano na waandishi wa habari ingawa mikutano hii nayo inapaswa kuepekuwa au waendapo kusali katika nyumba za Ibada.
Vile vile ikitokea wanaenda kufanya manunuzi basi wavae mask ili kuhamasisha wananchi wengine kuvaa mask.
Na ikiwezekana, mfano Rais, anaweza kufanya shopping ya makusudi tu huku akiwa amevaa barakoa lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi watumie barakoa (hata kuigiza kwa aina hii kuna tija).
Vile vile haitakuwa na maana kuwataka wananchi wavae barakoa huku viongozi wakionekana hadharani au kwenye vyombo vya habari wakiwa hawajaavaa barakoa.
Uongozi ni kuonyesha njia.
Ni ushauri katika kupambana na corona.