Ushauri katika wazo hili la kibiashara

Ushauri katika wazo hili la kibiashara

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wakuu habari?
Nina hili wazo la kufungua youtube channel ambayo content yake itakuwa mambo ya ujenzi lakini kabla ya kulitekeleza, naomba nipate mawazo yenu yatakayonisaidia nisipate hasara.

Timu yake itakuwa kama ifuatavyo:-
  • Mimi mwenyewe (CEO/chairperson)- kazi yake ni kutoa miongozo, vitendea kazi, ofisi, rasilimali fedha.
  • Mtaalamu wa IT- kazi yake ni kucheza na channel (youtube)
  • Mtaalamu wa ujenzi (civil engineer)- Presenter
  • Mchukua video (videographer) -kazi yake ni kurekodi video akiwa site
  • Mtaalamu wa sheria- kushughulikia vibali, na nyaraka zote za kampuni
  • Mtu wa mauzo- kuhakikisha fedha zote zilizowekezwa zinarudi kwa faida
Naombeni ushauri, huyu mtu wa mauzo atatumia njia zipi, kuhakikisha hii program inaleta fedha za kujiendesha na faida?
 
Mbona hujaainisha gharama inayotakiwa ukaiweka?

Pia kwa kuanza naona uko na team kubwa itakutia hasara mengine unaweza kufanya mwenyewe mpaka utakapokuwa mkubwa
 
Wakuu habari?
Nina hili wazo la kufungua youtube chanel ambayo content yake itakuwa mambo ya ujenzi, lakini kabla ya kulitekeleza, naomba nipate mawazo yenu yatakayonisaidia nisipate hasara.

Timu yake itakuwa kama ifuatavyo:-
  • Mimi mwenyewe (CEO/chairperson)- kazi yake ni kutoa miongozo, vitendea kazi, ofisi, rasilimali fedha.
  • Mtaalamu wa IT- kazi yake ni kucheza na chanel (youtube)
  • Mtaalamu wa ujenzi (civil engineer)- Presenter
  • Mchukua video (videographer) -kazi yake ni kurekodi video akiwa site
  • Mtaalamu wa sheria- kushughulikia vibali, na nyaraka zote za kampuni
  • Mtu wa mauzo- kuhakikisha fedha zote zilizowekezwa zinarudi kwa faida
Naombeni ushauri, huyu mtu wa mauzo atatumia njia zipi, kuhakikisha hii program inaleta fedha za kujiendesha na faida?
ni wazo Zuri! mtaji unao kiasi gani?? inatakiwa Leseni ya TCRA je unayo tayari?.kuna Hardwares zinahitajika za Studio kwa kuandaa vipindi na za kupeleka from studio to Youtube network je umeshaviandaa??.Channel promotion na kuifanya ijulikane na Walaji na watakaoleta matangazo ili upate pesa umejipangaje???. Nna weza kukusadia kwenye Design+hardwares zote na kwenye andaa vipindi ,marketing etc ni PM tuyajenge
 
Kuna Youtube Channel fulani nilikua nikifatilia kwa muda inaitwa "The Builders Home Tz". Ilikua ikiweka almost similar content. Kwa muda sasa sioni wakiweka new content. Unaweza pia kuitembelea ukajifunza kitu fulani cha kuboresha zaidi kwako. Kila la Heri Mkuu.
 
Mbona hujaainisha gharama inayotakiwa ukaiweka?

Pia kwa kuanza naona uko na team kubwa itakutia hasara mengine unaweza kufanya mwenyewe mpaka utakapokuwa mkubwa
Kwa mwanzo, mtu wa sheria na mauzo anaweza kupungua; kwa sasa nipo kwenye kupiga hesabu, kuhusu majengo na baadhi ya vitendea kazi vipo.
 
ni wazo Zuri! mtaji unao kiasi gani?? inatakiwa Leseni ya TCRA je unayo tayari?.kuna Hardwares zinahitajika za Studio kwa kuandaa vipindi na za kupeleka from studio to Youtube network je umeshaviandaa??.Channel promotion na kuifanya ijulikane na Walaji na watakaoleta matangazo ili upate pesa umejipangaje???. Nna weza kukusadia kwenye Design+hardwares zote na kwenye andaa vipindi ,marketing etc ni PM tuyajenge
Wazo bado liko mezani, kuhusu leseni hakuna shida itatafutwa, jengo lipo tayari,na baadhi ya vitendea kazi vipo; kwa sasa natathmini nitapataje faida, na ni kwa muda gani na kwa njia zipi?
 
Kuna Youtube Channel fulani nilikua nikifatilia kwa muda inaitwa "The Builders Home Tz". Ilikua ikiweka almost similar content. Kwa muda sasa sioni wakiweka new content. Unaweza pia kuitembelea ukajifunza kitu fulani cha kuboresha zaidi kwako. Kila la Heri Mkuu.
Nashukuru nitaifuatilia, changamoto za biashara zinaitaji uvumilivu, unaweza kuwa unapata hasara mara kwa mara, na kama final destination ukui-plan vizuri, inakuwa ni ngumu kuivumilia.
 
1. Timu umechukua ya watu wengi sana jitahidi kwa mwanzo basi wasizidi watu wawili jumla na wewe muwe watatu IT na videographer anawez kushika mtu mmoja, mwanasheria hana umuhimu sana kwa sasa hakimu wako mkubwa ni google, nafasi ya muhasibu unaweza kuicover wewe mwenyewe. Lengo kubwa ni kucontrol gharama vizuri

2. Angalia target audience ni ipi, kama lengo lako ni kuifikisha hii project kwa watanzania basi jaribu kufikiria mara mbili au hata upitie pitie content za watu wanao piga kazi na youtube kwa bongo (Ushauri binafsi au mtazamo wangu kwa watz hawana morale sana na vitu vya serious huwa wanapenda sana habari zinazo husu makalio, vichekesho, udaku na ujinga mwingine)

3. Jaribu kupitia sheria za youtube(adsense) na uzizingatie kweli kweli kwa sababu google wako very strictly kwenye suala la content, one mistake wanadisable acc yako kabisa na hawana hata sehemu ya kupeleka malalamiko.

Kama nitapata muda nitaendelea mkuu
 
apo kupiga pesa nafkili nimatangazo na streamers na hapo ni baada ya chanel yako kuwa famous... Pia unaweza kuwa nakamradi kako ka uuzaji wa vifaa kupitia iyo chanel uwe unajipigia chapuo
 
Kwa uelewa wangu mdogo wa mambo za online business. ..
1) Hizi biashara zinahitaji sn data, yaan data ndio hela yenyewe. Na data kuzikusanya inahitaji muda. Data nazozizungumzia hapa ni views sijui wengine wanaita viewers (wataalam watatusaidia) utahitaji subscribers, likes and even shares for channel growth. Mana YouTube wanakiwango chao cha numbers of data wanachokihitaj ili uweze kulipwa...ntarudi kwa mengineyo....
 
Back
Top Bottom