Ushauri: Kichanga wangu analia sana usiku

Ni kawaida sana msimbembeleze kwa kumtikisa Mimi Nina mapacha wa like nashukuru mungu hawalii sana watu wanasema Mtoto wa kiume Ndio Analia zaidi kuliko wa kike.
 
Gesi huchangia watoto kulia sana kwani wanapata maumivu katika tumbo- Azingatie anapomnyonyesha mtoto ahakikishe weusi wa ziwa umeingia katika mdomo wa mtoto yaani mtoto asinyonyeshwe chuchu tuu hii itasaidia kuepuka gesi kuingia tumboni kupitia mdomoni
Pili Kila mtoto akinyonya ahakikishe amebeua amweke begani amtikise taratibu mpaka abeue,
Joto linachangia mtoto kulia mpunguzie nguo mambo ya kumvika sweta,kanga,babyshow,shuka,blanketi hapana hii itachangia kumpa mtoto nimonia
Tatu: Mwambie Mungu akulele mtoto muombee mara zote mtoto wako kuna vitu vya rohoni huwa vinaendelea watoto wadogo wanauwezo wa kuona YESU pekee ndiye amfunike
Nne:Mtoto hashibi una maziwa mepesi ambayo muda mfupi tuu mtoto anapata njaa hivyo kuna wajumbe wamechangia juu namna ya ulaji wako uji ,mtori ,uji wa mchele nk.
Mwisho sio mbaya kumpa maji ya vugu vugu mtoto hata vijiko viwili .Japo wanasema maziwa ya mama yana maji lakini hata vichanga ni binadamu jamani.
 
miezi 6 ya kwanza mtoto haitakiwi apewe chochote zaid ya ziwa la mama.

Theory au nadhalia hiyo mkuu

1. Kuna wamama maziwa hayatoki

2. Kuna watoto mama zao hupoteza maisha kwa sababu mbalimbali

3. Kuna wanandoa huteleza na mama kushika mimba mpemaa......

Nk

Je unampa nini?

Kama umezaa na kulea utanielewa

Kama hujazaa huwezi nielewa

Waliotengeneza maziwa hayo wanaakili timamu

Chukuwa ushauri wa bure.
 
Mwanao anasumbuliwa na gesi. Pamoja na njaa. Hashibi maziwa ya mama yake. Huwa yanaisha mchana. Na akiwa ananyonyesha ile chuchu ya mama yake aibugie yote isiiweke jujuu inaingiza hewa wakati ananyonya. Ndio maana anapata gesi tumboni. Pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…