SoC01 Ushauri: Kidato cha nne wanaopata Div 0 hadi 4 wapangiwe vyuo vya Ufundi moja kwa moja

SoC01 Ushauri: Kidato cha nne wanaopata Div 0 hadi 4 wapangiwe vyuo vya Ufundi moja kwa moja

Stories of Change - 2021 Competition

kipenseli2021

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2021
Posts
1,390
Reaction score
1,431
Kulingana na mabadiliko ya Uchumi na ukiangalia nchi yetu tangu awamu ya Tano tupo kwenye Sera ya viwanda,maendeleo ya viwanda yanakwenda sambamba na mambo yafuatayo

1:Miundo mbinu kama Barbara
2:Rasilimali watu
3:Malighafi

Lakini naomba niweke mkazo kwenye rasilimali watu ,viwanda vinahitaji sana rasilimali watu ambao wengi waho ni mafundi wa level ya Artisan au Technicians ambao ni mazao ya Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC).

Kwa kuzingatia hitaji hill basi napendekeza njia ifuatayo kusajiri wanafunzi wa kidato cha nne wanao maliza mtihani who na kufanikiwa kupata kuanzia Div 0 hadi Div 4 kundi hili ni kipaumbele lakini pia hata wale watakao penda wenyewe

Pendekezo:Njia ya kuwasajili

1: Serikali iwasajiri au kuwapangia moja kwa moja wanafunzi waliomaliza na kupata au kufaulu kwa kiwango hicho cha kuanzia Div 0 hadi Div 4 kwenda moja kwa moja kwenye Vyuo vya Ufundi vilivyo chini ya VETa na vile vya Maendeleo ya Wananchi (FDC)

Je kwanini serikali iwapangia moja kwa moja

1:Kuongeza morali kwa wanafunzi hawa maana watajiona sawa na wenzao wanopangiwa katika vyuo vilivyo chini ya Nacte moja kwa moja

2: Kuwapa nafasi hata wale wasiokuwa na taarifa kuhusiana na mafunzo ya Ufundi,hii itasaidia hata wazazi/walezi waho kuwatilia mkazo hili waende kusoma

3: Kuondoa mianya ha upendeleo katika kuwasajiri wanafunzi katika vyuo vya Ufundi

4: Kutasaidia vyuo kupunguza gharama za kutangaza kozi maana wataletewa wanafunzi moja kwa moja

Hitimisho

Nashauri serikali kutilia mkazo katika elimu ya ufundi na kuwashauri wadau mbalimbali wawekeze katika elimu ya ufundi,pia serikali iwasajiri wanafunzi moja kwa moja kwenda kwenye vyuo vya ufundi wale wenye ufaulu wa wastani

Imeandaliwa na Kipenseli
 
Upvote 5
Back
Top Bottom