Ushauri: Kipi bora kati ya kupanga na kukaa hostel?

Ushauri: Kipi bora kati ya kupanga na kukaa hostel?

Allydasmartboy001

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Posts
604
Reaction score
218
Naombeni msaada kuhusu mazingira gani mazuri kwa kujisomea kati ya kupanga au kukaa hostel za chuo ili kupata matokeo chanya? Tukianza kwa gharama, nasoma chuo ambacho hostel zake ni laki 4 kwa mwaka wakati chumba cha kupanga kinaanzia elfu 20 hadi elfu 30 kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni 240K hadi 360.
 
Mkuu mbona kama bado hujaweka details zakutosha mfano, chuo ni chuo gani?, mkoa gani?, na level gani ya elimu mf. Certficate, diploma, degree au masters?

Embu ongezea ongezea details mkuu

Ila kwa haraka haraka, kama chuo ni Dar na level ni certficate/dploma kaa hostel mkuu ila kama ni degree mwaka wa kwanza na wapili semista ya kwanza kaa hostel ila ukiingia semista ya pili au mwaka wa tatu tafuta gheto

Ila sasa napo inategemea na chuo sababu kuna vyuo vina hostel huko huko na kuna vyuo havina hostel kabisa.

Kwa vyuo vilivyopo mkoani kwa level zote unaweza ukaamua kupanga kabisa ila kama umeupenda mkoa husika au una plan yakubaki huko muda mrefu.

Sababu za kuanzia histel kwa Dar ni garama za maisha na uzoefu wa hili jiji, ukiwa mgeni kama mimi utajikuta msimu wa mvua hauendi chuo kabisa [emoji23]Mkuu ila embu weka details zaidi mkuu
 
Ufaulu ni akili zako tu kokote unaishi wether ni hostel or mtaani though kupanga kunakusaidia kutanuka kiakili na kimatendo pia
 
Inategemeana na chuo, mahali na mtu mwenyewe
 
Umeuliza swali la msingi hata me pia nilitaka kupanga Ili kuepuka gharama lakin nilishauriwa kuwa nisipange sababu Ni first year maana nako kupanga Kuna hasara zake Kama ukiwa hauko serious na masomo
 
Kwa hiyo ulivoshauriwa ukikaa hostel unafaulu kiwango cha juu!

Ujinga ujinga tu kasome na usivae vinguo tufupi.
Umeuliza swali la msingi hata me pia nilitaka kupanga Ili kuepuka gharama lakin nilishauriwa kuwa nisipange sababu Ni first year maana nako kupanga Kuna hasara zake Kama ukiwa hauko serious na masomo
 
kufaulu ni wewe mwenyewe utakavyojituma. Mm enzi zangu sikuweza kabisa kusomea chuo au library na hata nilipokuwa ghetoo pia sikuweza kusoma nikiwa nimekaa kwenye kiti na meza..mara nyingi mm nilikuwa nikisoma nikiwa kitandani na nilifaulu vizur sanaa..

So ni wewe mwenyewe utakavyo jitume , ila kokote pale unaweza soma na ukafaulu iwe ghetto kwako umepanga au Hostel...
 
Back
Top Bottom