Ushauri: Kubadili mfumo wa gari ili litumie gesi

Ushauri: Kubadili mfumo wa gari ili litumie gesi

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Nilipewa elimu kuwa ukitaka kupunguza gharama ya matumizi ya gari basi ni vema ukaibadili na iweze kutumia mfumo wa gesi. Nikaelezwa kuwa ukijaza gesi ya Tshs. 17,000 unaweza kusafiri kilomita zaidi ya 200.

Nimefanya mahesabu kati ya matumizi ya mafuta na kila kukicha bei yake inapanda na gesi nikaona kuwa afadhali nibadili mfumo wa gari langu ili itumie gesi.

Nimeelezwa kubadili mfumo mzima wa gari kutoka kwenye matumizi ya mafuta na kwenda kwenye gesi itanigharimu Tshs.1.5 millioni.

Mimi ninakaa Mwanza je utaratibu huu una faida?.

Je, nitapata fundi hapa Mwanza wa kubadili mfumo huo?.
 
Nilipewa elimu kuwa ukitaka kupunguza gharama ya matumizi ya gari basi ni vema ukaibadili na iweze kutumia mfumo wa gesi. Nikaelezwa kuwa ukijaza gesi ya Tshs. 17,000 unaweza kusafiri kilomita zaidi ya 200. Nimefanya mahesabu kati ya matumizi ya mafuta na kila kukicha bei yake inapanda na gesi nikaona kuwa afadhali nibadili mfumo wa gari langu ili itumie gesi. Nimeelezwa kubadili mfumo mzima wa gari kutoka kwenye matumizi ya mafuta na kwenda kwenye gesi itanigharimu Tshs.1.5 millioni. Mimi ninakaa Mwanza je utaratibu huu una faida?. Je nitapata fundi hapa Mwanza wa kubadili mfumo huo?.
Nipo kiti cha mbele Namimi kupata elimu
 
Hapo Mwanza upatikanaji wa Compressed Natural Gas ni kama Dar ?, Pili sidhani kama wanabadilisha moja kwa moja wanafanya inakua dual (yaani unaweza kutumia mafuta au gesi)
 
MWANZA bado hawajafunga sheli za Gesi! ipo Dar pekee kwa sasa!

CNG ni nzuri sana unapunguza gharama kwa 60%
 
kwani utazikwa nalo babu!? lakini Gesi ni natural haiharibu engine na ni bei chee! badala ya 100,000 petrol unatumia 40,000 kwa gesi
Ni sawa na kubadili injini ya cc4800 na kuweka ya cc 2000; Aliyebuni kiwandani hakukosea kuweka hiyo injini
 
Wengi hapa naona hawaelewi mfumo wa gesi ulivyo na namna unavyofanya kazi watakupa majibu tofauti kabisa, ila watumiaji wakubwa mpaka sasa wa hii ni maderea Uber, Bolt, baadhi wenye magari binafsi na magari makubwa ya Dangote ukiwapata hawa watakupa maelezo mazuri pamoja na uzoefu wao. Nakushauri kama ni mtu wa Dar nenda DIT utapewa elimu kamili kuhusu hii pia kwa Dar ndio najua wana vituo viwili vya kujazia NCG
 
Nilipewa elimu kuwa ukitaka kupunguza gharama ya matumizi ya gari basi ni vema ukaibadili na iweze kutumia mfumo wa gesi. Nikaelezwa kuwa ukijaza gesi ya Tshs. 17,000 unaweza kusafiri kilomita zaidi ya 200.

Nimefanya mahesabu kati ya matumizi ya mafuta na kila kukicha bei yake inapanda na gesi nikaona kuwa afadhali nibadili mfumo wa gari langu ili itumie gesi.

Nimeelezwa kubadili mfumo mzima wa gari kutoka kwenye matumizi ya mafuta na kwenda kwenye gesi itanigharimu Tshs.1.5 millioni.

Mimi ninakaa Mwanza je utaratibu huu una faida?.

Je, nitapata fundi hapa Mwanza wa kubadili mfumo huo?.
Ukifunga gesi jiandae gari kupoteza nguvu kwa 40%
 
Back
Top Bottom