Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,959
- 24,935
Kwanza niseme wazi mimi Mr Zero IQ ni shabiki kindaki ndaki wa timu Kongwe sana hapa nchini "Young Africa ", kupitia yeye ndio ikazaa timu ya Sunderland na atimae ndio Simba Sc ya sasa ambao wamekuwa watani wetu wa jadi sio ndani tu ata nje ya Uwanja.
Ukitoa porojo za Ndugu @Gentamycin hapa jukwaani na zile za manara kule mtandaoni, Young Africa inabaki kuwa ndio timu pekee yenye historia kubwa ya Soka hapa nchini na barani Africa.
Ngoja niende direct kwenye dhumuni la mada yangu. Ni kwamba ningependa kutoa ushauri wangu kwa Viongozi Tukuka wa Club kongwe ya Young Africa(yanga) pamoja wasimamizi wa utengenezaji wa jezi za timu GSM,kuelekea siku ya mwananchi mwaka huu wa 2020.
Najua wazi siku hii pendwa ya wananchi ndio siku pekee inayokwenda sambamba kabisa na tukio Muhimu la kutambulisha Uzi mpya wa Timu pamoja na wachezaji wa msimu mpya wa 2020/2021.
Ushauri wangu ni mdogo tu na itapendeza zaidi kama utafika kwa viongozi tukuka wa club hii kongwe na kuujadili ni kwamba.
Siku hiyo pekee na muhimu kwa wananchi kusiwe na kiingilio chochote pale uwanja Wa mkapa isipokuwa wazalishaji na wasimamizi wa Jezi GSM Watengeneze Jezi za kutosha pea nyingi wawezavyo ili siku hiyo ya wananchi ikifika hizo jezi ndio ziwe kiingilio cha pale uwanja wa mkapa.
Hapa nitoe summery ni kwamba zitolewe bei elekezi za jezi kabisa kama ni 35K(elfu 35) per kit. Alafu GSM watengeneze duka(kituo kidogo cha kuamishika) pale getini kabisa ya uwanja. Shabiki akija ananunua Jezi anapewa risiti anafunguliwa geti anapita, yaani hiyo jezi ya msimu mpya wa yanga ndio iwe Gate pass yake, na kununuliwa kwake iwe ni pale getini tu.
Yanga ikifanya hivyo kwanza itauza jezi nyingi na kujipatia mapato kuliko ata mapato wanayotegemea kupata kwenye kiingilio,
Pili serikari itapata kodi yake stahiki kutokana na kila jezi itakayouza inatolewa risiti.
Tatu itafanya siku hiyo pendwa ionekane ni siku ya tofauti na ya kupendeza zaidi huku majukwaani ikipambwa na jezi nzuri za timu ya wananchi Yanga.
Nne na mwisho ni kwamba itasaidia sana kuzitangaza jezi hizo mpya za timu ya wananchi Young Africa msimu huu wa 2020/2021.
Asanteni