Ushauri kuhusu afya: Maumivu ya kifua yananisumbua (2)

Ushauri kuhusu afya: Maumivu ya kifua yananisumbua (2)

Chagaboy93

Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
14
Reaction score
8
Wakuu habarini.

Mwendelezo:

Ninaomba msaada kwa anayeweza kunishauri. Nimekuwa nikipata maumivu ya kifua eneo la katikakati ya kifua kurudi chini zinakoishia mbavu. Mara nyingi maumivu haya husikika upande wa kulia wa kifua pia.

Nimesha-attend hospital mbalimbali nikafanya vipimo vya X-Ray mara mbili, CT Scan nimefanya Muhimbili mwezi ulopita, Nilishafanya vipimo vya moyo, Damu nimepima lakini mpaka sasa sijajua tatizo ni nini. Nimekuwa nikienda hospital wananiandikia tu dawa Omaprazole na Anti-acid nyinginezo lakin bado shida yangu haishii!!Ninaishi kwa hofu kubwa mno. Muhimbili/Ekenywa hospital vipimo vimebainisha nina vidonda vya tumbo. Ila hivi vidonda ninaamini vimetibuka kutokana na msongo wa mawazo nilionao kwasababu ya huku kuumwa pasipokujua tatizo.

Muhimbili wamenipa dawa za Kemoxyl+f na Elogyl dozi ambayo nakaribia kumaliza bila nafuu yoyote.Pia kuna hali ya maumivu yapata wiki mbili sasa kwnye koo la kushoto ambapo ninapata changamoto ya kumeza. Pia yapata wiki moja ambapo nimekuwa ninaenda chooni zaid ya mara tatu kwa siku, na ninatoa choo cha rangi ya brown au kahawia.Kinyesi kinakuwa siyo kigumu sana(siharishi).

Naombeni msaada wa ushauri jamni. Age yangu ni 29yrs. Sinywi pombe kali, sivuti sigaara

Pia, soma: Msaada wa kiafya: Maumivu ya kifua yananisumbua (1)
 
Acha tu tiba mbadala waendelee kujipigia mihela mtaani, sasa MNH hii Kemoxyl+F (FLUCAMOX) na Metronidazole ni za nini?
 
Tatizo lako linaonekana unazalisha acid nyingi ambayo ndo inakusababishia maumivu ya kifua(burning pain)
So provisional diagnosis ~GERD or Peptic Ulcer d’se(PUD)

Nenda karudie kupima ulcers (stool H.pylory Antigen)

Kama ni kweli basi kanunue Heligo Kit + ant-Acid(pantoprazole) utumie hakika zitakusaidia
 
Shukran mkuu sasa je hizi kemoxy+f na elogyl ninazotumia siyo za kutibu hilo tatizo?Mara ya kwanza nilipoumwa vidonda vya tumbo nilitumia Helgo kit nikapona vidonda but ishu ya kuumwa kifua ilianza wiki mbili baadae na mpaka leo imedumu mwaka sasa
 
Ngoja waje watushauri!Mimi dalili zote ulizotaja ninazo!Ila Mimi tumbo linajaa,mguu wa kushoto nikitembea nahisi kichomi katika sehemu ndogo ya kushoto kiunoni.Vipimo vyote nilivyopima havionyeshi ugonjwa!!!
 
Pole sana na wewe mku.Sina aman kabisa
 
Wakuu habarini.

Mwendelezo:

Ninaomba msaada kwa anayeweza kunishauri. Nimekuwa nikipata maumivu ya kifua eneo la katikakati ya kifua kurudi chini zinakoishia mbavu. Mara nyingi maumivu haya husikika upande wa kulia wa kifua pia.

Nimesha-attend hospital mbalimbali nikafanya vipimo vya X-Ray mara mbili, CT Scan nimefanya Muhimbili mwezi ulopita, Nilishafanya vipimo vya moyo, Damu nimepima lakini mpaka sasa sijajua tatizo ni nini. Nimekuwa nikienda hospital wananiandikia tu dawa Omaprazole na Anti-acid nyinginezo lakin bado shida yangu haishii!!Ninaishi kwa hofu kubwa mno. Muhimbili/Ekenywa hospital vipimo vimebainisha nina vidonda vya tumbo. Ila hivi vidonda ninaamini vimetibuka kutokana na msongo wa mawazo nilionao kwasababu ya huku kuumwa pasipokujua tatizo.

Muhimbili wamenipa dawa za Kemoxyl+f na Elogyl dozi ambayo nakaribia kumaliza bila nafuu yoyote.Pia kuna hali ya maumivu yapata wiki mbili sasa kwnye koo la kushoto ambapo ninapata changamoto ya kumeza. Pia yapata wiki moja ambapo nimekuwa ninaenda chooni zaid ya mara tatu kwa siku, na ninatoa choo cha rangi ya brown au kahawia.Kinyesi kinakuwa siyo kigumu sana(siharishi).

Naombeni msaada wa ushauri jamni. Age yangu ni 29yrs. Sinywi pombe kali, sivuti sigaara

Pia, soma: Msaada wa kiafya: Maumivu ya kifua yananisumbua (1)
Mkuu pole kwa maradhi yako uliyokuwa nayo na hujuwi chanzo cha maradhi yako ingawa umepima vipimo vya hospitali . Umeambiwa unayo maradhi ya vidonda vya tumbo vilivyotokana na stress ulizo kuwa nazo. Kwa ufupi wewe unayo maradhi ya elimu ya giza Uchawi na sio rahisi kwa vipimo vya hospitali kuonekana hayo maradhi ya elimu ya giza aka uchawi nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole Mkuu.
 
Shukran mkuu sasa je hizi kemoxy+f na elogyl ninazotumia siyo za kutibu hilo tatizo?Mara ya kwanza nilipoumwa vidonda vya tumbo nilitumia Helgo kit nikapona vidonda but ishu ya kuumwa kifua ilianza wiki mbili baadae na mpaka leo imedumu mwaka sasa
Kwaiyo tatzo la kifua umeshapona mkuu au bado linaendelea baada ya kutumia heligo kit
 
Mkuu pole sana kwa tatizo hilo.

Labda niandike kilichonisaidia mimi.
Kwanza kabisa nilipatwa na dalili kama zakwako nilipokuwa chuo Saut mwaka 2014 na niliteseka sana. Dalili zangu zilikuwa kali mno hadi maumivu yalisambaa hadi kwenye bega na mkono wa kushoto.Mara nyingine yalishuka hadi kwenye miguu na unyayo. Hospitali za bongo niliishia kupewa vitamin b12 na kuambiwa labda ni Acid reflux. Nilikata tamaa sana pale watu waliponimabia labda nimelogwa. Nilifikia mahali nikasema acha tu nikae hivyo. Maumivu yalikuwa mara nyingi yanakuwa makali mfululizo wa siku 5 hadi 6 masaa 24.

Mungu siyo athumani nilipata nafasi ya kuja abroad na ndipo nikaamua kulipa uziti tatizo hilo kwa sababu nina insurance. Nilienda hosiptali nikafanya vipimo mbalimbali kuanzia, full blood profile, glands,ct scan,mri ya kichwa na spine, cadiac stress test, ECG,angiogram,lumbar puncture na nyingine nyingi. Hawakuona chochote. Wakani refer kwa Chiropractor. Basically, Chiropractor aligundua kwamba nina muscle knots mgongoni na pia ribs cartilage zilikuwa zinatatizo wanaita (Costochondritis). Ebana ehh, tukaanza mazoezi ya mgongo, yapo mengi ila kuna hili moja ambalo aliponifanyia tu maumivu yaliondoka within dakika 4. Unalala kwa tumbo (hakikisha umelala sehemu flat, kama vile sakafuni, usilale kwenye godoro) kisha aku crack. Angalia video hii maana ni ngumu kueleza kwa maandaishi. Pia hakikisha unamwambia anaye ku krack afanye hivyo unavyopumua hewa nje.

Pole sana kwa uhandishi wangu, mimi siyo mwandishi mzuri ila natumaini utafaidika na nilichokiandika.
 
pole bro Kama ulishafanya vipimo vyote relax iyo Hali ni anxiety attacks ni hofu kuu kwamba unahisi una ugonjwa mkubwa ambao hauna so mwili nao unaadapt..as if unaugonjwa lakini sio kitu Kama ulishafanya vipimo vikibwa na hauna shida basi relax iyo Hali inaitwa gastric yaani unapata maumivu kifuani kutokana na acid inayotokana na hofu na stress so ulirelax baada ya mda itaisha labda karibu kupima h piroly ..then utafuata ushauri wa Dr..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu ,jaribu hii chukua vitunguu maji vikubwa kama vinne au vi 5 visage vizur upate rojo chukua asali mbichi changanya hakikisha asali iwe mara mbili yaan kama rojo litakuwa mfano vijiko 10 bas asali iwe vijiko 20,tumia kulamba vijko 3 ktwa mara 3 ndani ya wiki moja uspoona mabadiliko nicheki tena kwa muda wako au urudi hapahapa
 
Ngoja waje watushauri!Mimi dalili zote ulizotaja ninazo!Ila Mimi tumbo linajaa,mguu wa kushoto nikitembea nahisi kichomi katika sehemu ndogo ya kushoto kiunoni.Vipimo vyote nilivyopima havionyeshi ugonjwa!!!
Umeshawahi pima amoeba?
 
Tayari!Amoeba alinitesa sana kwa miaka minne mfululizo!Dawa nilitumia za kutosha baadae kikaja kichocho cha tumbo
 
Back
Top Bottom