Ushauri kuhusu Alteza

GX 100 ni unyama
 
Wakuu ushauri wenu nataka niishi umu kwny teza beam 2000 yahama mwenye uzoef na hizi gari plz ushauri kwenye suala la mafuta na service kwa ujumla View attachment 2450205
Kama ni hiyo hiyo ya kwenye picha, hiyo engine ni 1G. Inahitaji matunzo tu. Gari ni ngumu vya kutosha. 1G inavumilia shida kuliko 3S, na spare za 1G zimejaa kila kona (kumbuka 3S ya Altezza ni very special, ilitengenezwa kwa Altezza tu, sio the same 3S ya kwenye Rav4 na wengine).

Japo ina common problems, kama bush za mbele kuisha na mafundi wakishafungua miguu wanashindwa kurudisha kwenye aligment. Pia ziko chini, hata ukiinua bado utakwaruza tu kama hauko makini.

Kwa hiyo namba yake, lazima ujiridhishe na utunzaji wa mmiliki wa mwanzo. Maana ina karibu 10yrs hapa kwetu.
 
Injini zote nzuri mkuu!

Zimezidiana power output.. 1G ni I6 na inazalisha around 170hp while 3s ni I4 inayozalisha 200+ hp.

Utofauti huo umesababidha hata consumption ya 3s iwe juu zaidi ya 1G..
Consumption ya 3s kwa lita ni km ngapi mkuu?
 
Shida ni nini mkuu,halafu kuna tofauti gani ya uimara na consumption kati ya engine ya 3s fe iliyopo kwenye noah,rav4 old n.k na 3s ge ya kwenye altezza?
3S GE ya Altezza imekuwa tuned na Yahama kwa ajili ya Altezza tu. Inaitwa Black top. Ina performance kubwa. Ni imara ila spare parts zake ni chache. Nyingi haziingiliani na 3S FE wala 3S GE ambazo sio Black top. So lazima upate parts kutoka kwa 3S GE Beams.

Consumption kwa mjini ni nzuri kuliko 1G. Kimeo chake, hakikisha unabadilisha timing belt on time. Usisubiri ikatike.
 
Shukran mkuu
 
Kikawaida timing belt inahitaji itumike kama km ngapi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…