Ushauri kuhusu biashara ya bodaboda ‘za mkataba’

Ushauri kuhusu biashara ya bodaboda ‘za mkataba’

hayolae

Senior Member
Joined
Sep 28, 2015
Posts
180
Reaction score
865
Salama ndugu zangu?

Kama ilivyo ada JF halishindikani jambo.

Nina mpango wa kununua bodaboda na kuwapa vijana kwa mkataba. Wakimaliza mkataba zinakua mali yao.

Kwa wenye uzoefu na biashara hii naomba mnipe changomoto na mbinu pamoja na mawazo mbalimbali yanayohusiana na kazi hii ili nisikwame.

NATANGULIZA SHUKRANI.
 
Ukishanunua nambie nikupe jamaa yangu kabisa ustadhi hope mtawezana hana makuu, kama uko tayari utanicheki dm
 
Biashara pasua kichwa hiyo ni sawa na kujaza maji kwenye tenga.
Ipo hivi pikipiki aina ya boxer inauzwa mil 2.8, hesabu ya siku unaletewa elfu 10 na mkataba kwa kawaida ni miezi 13..ukiwa unaletewa kila siku elfu 10 kwa mwezi utakuwa umeingiza laki 3,laki 3*13=3900000
3900000-2800000=1100000
Faida kwa mwaka mzima unapata mil 1.1
1100000÷13=84615...
Unatoa mil 2.8 mfukoni halafu kwa mwezi faida unaingiza elfu 84615 kama sio utahaira ni nini? Na mwisho wa siku pikipiki inakuwa sio yako tena

NB: Hapo bado haujapewa taarifa ya kuibiwa pikipiki, service ikiwa kubwa ni juu ya boss
 
Biashara pasua kichwa hiyo ni sawa na kujaza maji kwenye tenga.
Ipo hivi pikipiki aina ya boxer inauzwa mil 2.8, hesabu ya siku unaletewa elfu 10 na mkataba kwa kawaida ni miezi 13..ukiwa unaletewa kila siku elfu 10 kwa mwezi utakuwa umeingiza laki 3,laki 3*13=3900000
3900000-2800000=1100000
Faida kwa mwaka mzima unapata mil 1.1
1100000÷30=36660....
Unatoa mil 2.8 mfukoni halafu kwa mwezi faida unaingiza elfu 36 kama sio utahaira ni nini ? Na mwisho wa siku pikipiki inakuwa sio yako tena
Umekosea hesabu rudia tena.
 
Biashara pasua kichwa hiyo ni sawa na kujaza maji kwenye tenga.
Ipo hivi pikipiki aina ya boxer inauzwa mil 2.8, hesabu ya siku unaletewa elfu 10 na mkataba kwa kawaida ni miezi 13..ukiwa unaletewa kila siku elfu 10 kwa mwezi utakuwa umeingiza laki 3,laki 3*13=3900000
3900000-2800000=1100000
Faida kwa mwaka mzima unapata mil 1.1
1100000÷13=84615...
Unatoa mil 2.8 mfukoni halafu kwa mwezi faida unaingiza elfu 84615 kama sio utahaira ni nini ? Na mwisho wa siku pikipiki inakuwa sio yako tena

NB:hapo Bado haujapewa taarifa ya kuibiwa pikipiki, service ikiwa kubwa ni juu ya boss
Sasa kipi bora, kuwapa vijana wakuletee elfu tano au elfu sita kwa siku. Bodaboda iendelee kuwa yako na matengenezo yote juu yako au hii ya mkataba matengenezo yote juu yake.???
 
Hizo ni biashara za watu wavivu vinginevyo watu wenye vyanzo vingi vya mapato wanaamua kudiversify kupunguza risk.
Wengine sio uvivu huenda hawashauriwi kufanya kazi hiyo kutokana na matatizo ya kiafya
 
Kuna njia naitumia na inanilipa vizuri sana....ngoja niweke hapa....

Mimi huu ni mwaka wa 2 huwa nanunua pikipiki used kwa mil 1.5 hadi 1.7 hivi..... nimepitia bodaboda 4 hadi sasa

Hizi pikipiki natoa kwa mkataba wa miezi 9 tu baada ya hapo inakuwa ya kwake.....

Hesabu 10 × miezi 9 (270) hesabu ya kichwani ilikuwa inakuja 2,700,000 laki 3 toa changamoto nyingine za service ndogondogo na hapo service nyingi huwa anapiga mwenyewe sababu pikipiki ni ya kwake.....ila mimi nimewatengea laki 3 ya service au janga lolote lile kuwasupport...

Hapo huwa inabakia kama laki 9 (900000) na nina bodaboda 2 .pia nina kipato kingine hivyo bodaboda huwa inanipa hela ya akiba tu....

So mara ya kwanza faida ilikuwa mil 1.9 ndani ya hiyo miezi 9 kwa mtaji wa mil 3... mara ya pili bado mkataba unatembea

Biashara zote ngumu, sio mbaya kufanya na sio kujaribu. Hapo ukipoint boda za mil 1 kwenda mil 1.3 faida inakuwa kubwa etc...

Angalizo bodaboda used nyingine za wizi, ununue upewe document au ununue kwa madalali official kidogo afadhali
 
Mimi niliwaambia hesabu 8000 kwa siku haina mwaka haina wala nini na chombo lazima kwa nyumba....
chombo zote zina GPC iba nakusomea albadir....
Sawa ni nununue daladala alafu baada ya miaka kadhaa Bus ya dereva huu utani kwetu hamna kabisa.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kuchukua milioni 2 laki 6 hadi 8 kununua TVS au Boxer na kumpa mtu akuletee elfu 10 kwa siku na baada ya miezi 13 pkpk sio yako ni matumizi mabaya ya akili. Risk ni kubwa sana, madereva wengine wanajichanja hadi viwembe wanakwambia imeibiwa. Siku hizi hata GPS mwizi akishirikiana na dereva wanafanikiwa. 2.8 mil ni pesa nyingi sana waweza fanya mengi kuingiza pesa nyingi tu. Nakushauri jipe muda ufanye research, mambo ya kufanya na 2.8 au 5.6 ya pkpk 2 ni mengi sana.
 
Back
Top Bottom