Ushauri kuhusu biashara ya kuuza dawa (pharmacy) Baridi

Ushauri kuhusu biashara ya kuuza dawa (pharmacy) Baridi

boazi kiwelu

New Member
Joined
Aug 13, 2015
Posts
4
Reaction score
0
Habari za muda wapendwa,

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mjasiliamali niko mkoa wa Dar es salaam naomba kupata a,b,c za namna yakufanya hii biashara ya kuuza dawa yaani famasia. Ni nini kinatakiwa, vigezo na Je, kwa wale wenye experience initial cost (capital) inaweza kwenda mpaka shiling ngapi?

Natanguliza shukrani.

Naomba mnifumbue macho kwenye hili.
 
Mimi nina interest pia. Wajuzi tunaomba msaada
 
mm pia nina interest na hii biahsra ya dawa baridi, mwenye ufumbuzi atutatulie plzz
 
Habari za muda wapendwa,

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mjasiliamali niko mkoa wa Dar es salaam naomba kupata a,b,c za namna yakufanya hii biashara ya kuuza dawa yaani famasia. Ni nini kinatakiwa, vigezo na Je, kwa wale wenye experience initial cost (capital) inaweza kwenda mpaka shiling ngapi?

Natanguliza shukrani.

Naomba mnifumbue macho kwenye hili.
Kesho nikipata muda nitawafafanulia.

Ni biashara nzuri ila ina changamoto zake kama kawaida.

Kikubwa upate location nzuri yenye watu.

Inatakiwa iwe walau mita 150 toka kwenye pharmacy nyingine.

Iwe na ukubwa wa 30sqm.

Kabla ya kuanza kukarabati au kulipia fremu nenda baraza la pharmacy kama uko Dar es Salaam.

Kama uko wilayani fika kwenye ofisi ya mfamasia wa Wilaya atakuhudumia.

Utaandika barua kuwaomba wakufanyie site visit waone kama eneo linafaa kuwekwa pharmacy.

Wakitembelea na kujiridhisha watakupa barua inayokuruhusu kuendelea na ukarabati wa standard zinazotakiwa.

Ukisharuhusiwa utakarabati na kuweka shelves, sehemu ya stoo, utaweka Air condition, sehemu ya kutunza dawa hatari, friji ndogo , viti vya wateja, watoa huduma n.k.

Ukishamaliza kukarabati unawapa taarifa wanakuja kukagua mara ya pili, wakiridhika na ukarabati kwa mujibu wa viwango vyao basi wanakuandikia palepale kwenye fomu zao kuwa unaruhusiwa sasa kuomba kibali cha kuendesha pharmacy.

Ukisharuhusiwa kuomba kibali basi kwa mujibu wa miongozo ya sasa anayeomba kibali ni mfamasia.

Inabidi utafute mfamasia mwenye degree na leseni pamoja na Pharmaceutical Technicians mwenye diploma na leseni.

Kwa sasa mishahara ya mfamasia ni kati ya 700,000 hadi milioni kutokana na makubaliano.

Mshahara wa Pharmtech ni kati ya 400,000 hadi 600,000 kutokana na makubaliano.

Ukishawapata na kuingia nao mkataba basi kinachofuata ni kujaza mikataba ya ajira maana ni attachment kwenye kuomba kibali.

Mkimaliza mfamasia anajaza fomu na kuweka attachment zinazotakiwa kisha anapeleka baraza la famasi au kwa mfamasia kama ni wilayani.

Hapo utaamua unataka famasi ya rejareja, jumla au jumla na rejareja.

Leseni ya famasi ya rejareja ni 450,000 kwa mwaka. Leseni ya jumla unaweza pata kwenye tovuti ya baraza la famasi pamoja na maelezo ya ziada.

Kiufupi gharama za miundombinu ya ndani inategemea na fremu umepata ikiwa kwenye hali gani.

Lakini ukarabati hadi unaoata leseni kwa famasi ya wastani ni kati ya 15m hadi 25m.

Kwenye dawa unaweza anza na 6 to 10m.
 
Back
Top Bottom