Hello wanajamii,
Nimefikiria kudeal na uuzaji wa vinywaji baridi (Jumla). Ila sio kama "Agent" bali muuzaji jumla wa kawaida nikiwa na stock ambayo sio ndogo sanaa na wala sio kubwa sana.
Nafikiria kudeal na vinywaji kama vya Coca Cola (take aways), bakhresa, sayona, jambo, Maji (bottled water), Malta, bavaria, n.k.
Natumaini itakuwa msaada kwa wengine pia kama tukipata maelezo kidogo kwa hints zifuatazo:
1. Kwa mimi muuzaji wa kawaida wa jumla, natakiwa kuchukua mzigo wangu kwa nani (distributor yupi)?
2. Ni vitu au njia gani ambavyo/ambayo unaweza kuviongeza au kuzingatia ili ufaidike na hii biashara?
3. Ni aina gani ya maeneo nayo paswa kufungulia hii biasahara?
4. Ni aina gani ya ushindani nitarajie kuupata na ni vipi naweza kupambana na huu ushindani?
5. Kwa makadirio, kwa aina hii ya biasahara tajwa, inatakiwa mtaji kiasi gani ili uingie bila kubabaika?
Tofauti na hints za hapo juu, Ni maelezo/ushauri/tahadhari gani nayopaswa kuzingatia katika hii biashara.
KARIBUNI WANA JAMII!
Sent using
Jamii Forums mobile app