Unakazi ngum sana kwenye hili na changamoto zake ni kubwa sana.
Kwanza nawasiwasi wa Uelewa wako wa Biashara za kupitia mitaji ya mikopo.
Unapotaka kukopa ni lazima uwe na mipango ya nini unafanya na kiasi gani kinatakiwa.
Sasa wewe unajenga Ofisi halafu pesa ya Bidhaa huna.
Then unasema kwamba una uhakika wa kuingiza elf 30,000 kama faida kwa siku.Hii ikimaanisha kwamba ni biashara yenye kuhitaji mtaji mkubwa kiasi.
Ungekuwa hujakopa ningekushauri kwamba usingekopa kwanza mpaka mchango wako kwenye Saccoss ufikie malengo yako.
Tatizo ulikurupuka kwa Tamaa,sasa ngoma imakaba shingo.
Tafuta mtu umpe wazo kisha mchangie mtaji,peke yako ni ngum sana na huwezi kupata pa kukopa labda uweke dhamana ya nyumba.
Na hata ukisajili kama kampuni kuna taratibu za watoa mikopo kuangalia mradi na mwaka gani umeanza na umezalisha kitu gani mpaka hapo au Bank statement na pia dhamana za Nyumba amabazo hupendelewa sana na mabank.So,sio Rahisi kabisa