Ushauri kuhusu Mabati ya Taishan, Kinglion na Sunbank

Ushauri kuhusu Mabati ya Taishan, Kinglion na Sunbank

NetworkEngineer

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2012
Posts
1,952
Reaction score
1,181
Habari,

Naomba kujua aliyewahi kutumia mabati ya kampuni hizo ubora wake ukoje, kwa eneo nililopo ndio bati zinazopatikana madukani sasa sijajua naenda wapi, ALAF najua wako bora ila bei yaoo inaniogopesha.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hiyo title aisee nilijua umetaja majina ya kihindi
 
Tanzania wewe nunua unapoweza. Sio kweli kwamba kila kitu ghali ni imara au kila kitu cha bei nafuu ni kibaya.
 
1. ALAF
2. SUNSHARE
3. TAISHAN

Source: Personal experience!
 
Nimeweka mabati ya Taishan, mwaka wa tatu sasa na sijaona tofauti. Ingawa wataalamu wanakwambia kuwa hakuna bati linalodumu katika rangi ile ile kwa miaka yote. Vitu kama upepo, joto, baridi, jua na mvua huwa vinaathiri rangi ya awali ya bati husika.
Screenshot_20231007-101835_1.jpg
 
Nimeweka mabati ya Taishan, mwaka wa tatu sasa na sijaona tofauti. Ingawa wataalamu wanakwambia kuwa hakuna bati linalodumu katika rangi ile ile kwa miaka yote. Vitu kama upepo, joto, baridi, jua na mvua huwa vinaathiri rangi ya awali ya bati husika.View attachment 2774203
Nyumba ya ukubwa huo imetumia bati ngapi?
 
Mkuu mabati bora ya muda wote ni ALAF kwingine unakuta roll la bat limeanza pata kutu kabisaa halafu linazalishiwa bat la rangi .
 
Nimeweka mabati ya Taishan, mwaka wa tatu sasa na sijaona tofauti. Ingawa wataalamu wanakwambia kuwa hakuna bati linalodumu katika rangi ile ile kwa miaka yote. Vitu kama upepo, joto, baridi, jua na mvua huwa vinaathiri rangi ya awali ya bati husika.View attachment 2774203
Miaka mitatu bado boma halijasogea hata kuweka grills tu. Aisee mkuu Komaa kutafuta hela! Miaka mitatu ni mingi mno!
 
Tuliezeka pamoja na jirani angu alitumia alafu migongo mipana nilitumia kiboko migongo midogo miaka miwili mvua ikinyesha kiboko Inan'gaa kuliko alafu.
 
Back
Top Bottom