Ushauri kuhusu Nissan Dualis

Naomba ufafanuzi kwanini nisiichukue wakati UMEISIFU ni nzuri..?

Kuhusu gearbox, huku vijiweni kwetu wanasema gearbox yake ni CVT ambayo wanasema ina kama 'maruhani!' [emoji1]
CVT ni gear box ambazo hazitaki kuchanganyiwa oil. Oil zake ni specific. Kuna CVT oil kwaajiri ya Toyota brands kama Toyota Lumion, Vits, Wish, Vanguard etc. Na ipo CVT ya Nissan Dualis, Nissan Xtrail, etc ambayo ipo specific kwaajiri ya gari husika.

Sasa zingatia kutochanganya oil ili uwe salama.
 
Asante kwa kutupatia uzoefu wako, mkuu.

Wengi tutafaidika! [emoji120]
 
Mpango wangu ni kuinunua ili niitumie.

Kwenye mipango yangu huwa sijitabirii kukwama,..

Lakini ikinitotokea dharura, na option pekee ya kunivusha ikawa ni kuuza mali yangu; nitaangalia ukubwa wa dharura yangu tu!

Mwenyezi Mungu atuepushe na mabalaa na mitihani ya kuturudisha nyuma kimaisha... aamiyn!
 
Tatizo la kiuchumi tusiilaumu gari [emoji1][emoji1]...

Tutafute hela!
 
Tutafute hela!

Tuache kulaumu magari!
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Shukrani sana mkuu, ubarikiwe!
 
Shukrani sana.

Wengi tunafaidika hapa! [emoji120]
 
Nunua Ila hakikisha kipindi chote unachokua unaimiliki uwe na paracetamol kopo 3 zile za kizamani moja unatembea nayo kwenye gar nyngne nyumban nyngne kazin
 
Nunua Ila hakikisha kipindi chote unachokua unaimiliki uwe na paracetamol kopo 3 zile za kizamani moja unatembea nayo kwenye gar nyngne nyumban nyngne kazin
Kwanini..?

Ina makelele sana yanaumiza kichwa au..?! [emoji1]
 

Shida kubwa inakuja ukiwa umepata fundi ambaye sio mzoefu na gari za Nissan. Hapo atakuharibia gari na utaona gari ni mbaya.

Kwa upande wangu pindi ilipokufa engine kuna fundi alishauri kufanya overhaul, ila hakuwa mzoefu na aliweka vifaa duni, tatizo halikupona, nilianza kuichukia gari. Ilifika mda nikatamani hadi kuiuza.

Na mara nyingi ukitaka kuuza kitu pindi una shida mnunuzi atakulalia tu, maana anajua unahitaji pesa.

Ila nikampata fundi mzoefu na tukarekebisha, na ikatulia.

Cha msingi uwe na hela ya kuihudumia, uweke vifaa original na ufanye service kwa wakati.

Tatizo kubwa nililopata ni hilo la engine, mengine madogo ni kama rubber boots, ABS sensor, taa za breki kuungua, bushes. Na nadhani hii ni kawaida hata kwa gari nyinginezo.
 
Ndio. Hata mimi natumia.
Gearbox yake mbovu kishenzi
Toleo gani na ulinunua kwa bei gani ?

Umenunua na kuitumia muda gani?!

Wewe ndie uliinunua na kutumia kwanza ama ulichukua mikononi mwa mtumiaji aliyeinunua, yaani swali langu ni gari imepita mikononi mwa watu wangapi kabla yako tokea iwe imported?!

Nipe history fupi ya service ya hiyo Nissan Dualis yako, ni lini ulianza experience shida ya gear box?!

Umefanya vipi diagnosis na kujua inashida?!

Ni muda gani umepita tokea ugundue tatizo na ni hatua gani umechukua hadi sasa?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…