Ushauri kuhusu sensa ya mwaka huu 2022

Ushauri kuhusu sensa ya mwaka huu 2022

Bundakisorya

New Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
3
Reaction score
3
USHAURI KUHUSU SENSA YA MWAKA HUU

Wasalaam ndugu zangu.

Nikiwa kama mwananchi nilikuwa nashauri jinsi mchakato wa sensa ulivyo mwaka huu.

Mchakato wa mwaka huu ni mpana na mrefu kitu ambacho kimefanya uhitaji wa makarani kuwa wengi na bajeti pia imekuwa kubwa.

Kitu kingine ni kuhusu maswali ambayo makarani watawauliza watu siku hiyo ni mengi sana na katika Kaya kwa mfano inaweza kuwa na watuwazima kuanzia kumi.

Watu hao wanatakiwa kuhojiwa kitu ambacho maswali ni mengi na muda nao ni mchache. Maswali yanasemekana ni kuanzia sabini kwenda juu hasa kwa wanawake.

Tatizo lingine siku ya sensa watu wameambiwa waende makazini. Hii itakuwa ngumu mno kwa makarani kupata data sahihi maana majumbani wanaobaki wengi ni wadada wa kazi na watoto au pasiwe na mtu kabisa.

Ushauri wangu.

Siku ya sensa watu wasiende makazini.

Sensa ijayo ihusishe wajumbe wa nyumba kumi kumi. Wajumbe hawa wa nawajua watu wao kwa ufasaha. Ili kurahisisha hili mtu anapoamia mtaani cha kwanza atoe taarifa kwa mjumbe kama ilivyo kuwa kipindi cha zamani na kujaza taarifa zake.

Halafu wajumbe wapewe mwezi mmoja kabla siku ya sensa kujaza taarifa za wakazi wake kwa kila Kaya kutokana na maswali yote yanayotakiwa kuhojiwa. Mjumbe kwa muda wa mwezi mmoja atagawa kwa nyumba kumi na kupata siku tatu kwa kila nyumba. Atakwenda kwa kila nyumba na kujaza watu wanaoishi kwenye nyumba hiyo au Kaya ambao ni wakazi wa kudumu.

Kisha siku ya sensa atakachofanya mjumbe ni kwenda kwa kila Kaya na kuuliza kama wale watu walioandikwa taarifa zao ambao no wakazi wa kudumu walilala ndani ya Kaya hiyo. Kama ni wale wale mfano watu kumi. Basi mjumbe anatia tiki tu.

Na kama kuna mtu hakulala siku hiyo hapo mjumbe anamkata.

Na kwa mgeni ambae amelala hapo mjumbe atachukua taarifa zake n kuziongeza.

Kwa kufanya hivi sensa itakuwa imefanyika kwa wepesi sana. Na itaokoa pesa nyingi mno.

Kinachotakiwa wajumbe wawezeshwe na maslai yao yawe mazuri kuliko yalivyo sasa.

Mfano kila mjumbe akapewa milioni moja tu kwa kazi hii ya sensa nadhani itakuwa vizuri.

Au makarani wangeshirikiana na wajunbe katika muda wote wa mwezi mzima kuliko hii ya siku moja mpaka sita
 
Wazo zuri, mkuu. Na kuna njia mbadala ambayo ni nyepesi na rahisi na fanisi zaidi. Ila sasa pesa zitapigwaje, mkuu? Angalia usije ukaingilia miradi ya watu, wenyewe wakakubutua.
 
Back
Top Bottom