Mkuu Hongera kwa kupata Subaru... Me sina hiyo Legacy.. Nina forester hivyo kwa uzoefu wa forester nilio nao in kwamba... Subaru haitaki magumashi, si kila fundi anaweza kutengeneza tu, service on time na oil nzuri, spea zake ziko juu sana Ila zinadumu, ni nzuri sana kwa Safari ndefu.. Kuhusu mafuta inategemea na uendeshaji wako na ukubwa wa engine, ukiwa mtu wa kurotate sana yaani unaenda 3,4,5 utaingiliwa tu hamna namna... Challenge iliyopo kwenye Subaru drivers ni kwamba tunapenda ligi na kusikiliza mnyama anapounguruma na kucheua, ukiendesha kawaida mafuta nayo yanakua kawaida Kama Magari mengine tu.