Ushauri: Kujenga nyumba mjini au nje ya mji

Promenthous

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
338
Reaction score
397
Habari wakuu,

Nahitaji ushauri wa wapi panafaa kujenga nyumba kwa ajili ya familia, option ya kwanza ni mjini,hii namaanisha sehemu ambayo haiko mbali na mjini na tayali kuna maendeleo kama barabara, umeme na huduma zingine za msingi,kero yake ni tayali kumeshabanana, utulivi hakuna na kiwanja sio kikubwa cha kuweza kujiachia au kufanya uwekezaji.

Option ya pili ni kujenga nnje ya mji,huku maendeleo bado hayajafika kama maji na umeme lkn barabara inafikika, uzuri wake kunautulivu, hali ya hewa nzuri na uwezekana wa kufanya uwekezaji mwingine upo kama vile kufuga, bustani n.k,kama ungelikuwa ni wewe ungechagua option gani na kwanini?
 
Nenda pembeni ya mji ila isiwe mbali sana. Kama
 
Nje ya mji ni pazuri kama una access ya usafiri wako binafsi, utapata eneo kubwa lakini pia baada ya miaka kadhaa pata endelea.
Mimi ni mmoja ya waliojenga nje ya mji changamoto kubwa niliyo nayo ni ukimya wa mazingira tu na ukosefu wa majirani kwa karibu lakini mengine yote yako poa sana.

Nb: Siku zote kwa mtu ndio mbali ila kwako huwa sio mbali, jenga nje ya mji uwahi eneo ndugu.
 
Nje ya mji,
Jenga msingi, kisha uuache tu.
Halafu rudi mjini ujenge nyumba wa wastani tu ya makazi.
Huduma za umeme na maji ni muhimu.

Kufikia miaka kadhaa mbele, huko nje ya mji kutachangamka,
Utaendeleza ule msingi na kujenga nyumba ya malengo yako,
Kisha mjini utaweka wapangaji.
 
N
i mji gani huo
 
Wazo zuri na la kimkakati[emoji106]
 
Ni kweli nnje ya mji pana utulivu,changamoto itahitaji kusubiri huduma za msingi hadi zifike.
 
Tafuta nje ya .ji penye umene, maji na barabara
 
jenga nje ya mji,siku hizi wachimba visima wengi,solar kibao, kama eneo ni kubwa panda miti ya mbao ya kutosha, after 15 years unakula pesa nyingi tu
 
Jenga mjini.... Then hamia.... kwa sasa


Then baada kidogo Jenga nje ya mji kwa ajili ya kustaafia huko na wajukuu kuja kula machungwa na maparachichi huko .... Then huku mjini utapangishaga.... Ikusaidie kununua samaki na matumizi madogo madogo siku za uzee wako.
 
Kwanini asijenge nyumba ya kustafia ya maana...ili pesa zijazo zifanye uwekezaji mwingine kama nyumba za kupangisha n.k
 
Ni kweli nnje ya mji pana utulivu,changamoto itahitaji kusubiri huduma za msingi hadi zifike.
Ni kweli la msingi unapaswa kujipanga na kuiweka akili tayari kukubali uhalisia, ukiwa na usafiri wako imara utaishi bila tatizo, hapa mjini kupata eneo kubwa ni nadra sana lakini pia inahitaji pesa nyingi ila nje ya mji utapata eneo kubwa ambalo unaweza fanyia mambo mengine mengi kadri siku zinavyokwenda, hata leo hii tunao waona wanamiliki maeneo makubwa mijini waliwahi zamani.
 
jenga nje ya mji,siku hizi wachimba visima wengi,solar kibao, kama eneo ni kubwa panda miti ya mbao ya kutosha, after 15 years unakula pesa nyingi tu
Kwakweli,uzuri wa nnje ya mji ni kuwa na eneo kubwa ambalo unaweza kufanyia mambo mengi,umeme ni wamuhimu lakini upatikanaji wa maji ndio muhimu zaidi
 
Ha ha ha kustafia[emoji16]kwaweli ukishakuwa mzee stress za mjini ni za kuzikimbia,mjini tunawaacha watoto na wapangaji.
 
Kwanini asijenge nyumba ya kustafia ya maana...ili pesa zijazo zifanye uwekezaji mwingine kama nyumba za kupangisha n.k
Ni sawa,hiyo nyumba ya kustafia ijegwe mjini kwenye huduma za msingi au huko nnje ya mji kwenye utulivu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…