mvukiyefrancis
Member
- Dec 8, 2012
- 31
- 8
Habari za kazi wana JF. Mimi nina kuku wa kisasa takribani 300. Ni wale wekundu na ni wa mayai. Tangu mwezi huu wa sita uanze, kuku hao wameacha kutaga kabisa. Ni leo tu nimeokota yai moja na lenyewe ni kadogo kama ka yai ka njiwa. Sielewi ni sababu gani hasa , kwani hapo nyuma walikuwa wanataga vizuri. Wana miezi 2 tangu waanze kutaga. Naomba ushauri wenu ndugu zangu kwani imenichanganya ukizingatia chakula cha kuku kila leo kinapanda bei. Ninaishi Mbeya eneo linaitwa ITUHA. AU je , kwa vile hivi sasa ni kipindi cha baridi, inaweza kuwa sababu? Mbona nina kuku wa kienyeji wana enda vizuri? Wana JF , NAOMBA USHAURI WENU, na MUNGU AWABARIKI SANA.