Ushauri: Kuna haja ya kujenga Kariakoo nyingine eneo la Mbezi Mwisho

Ushauri: Kuna haja ya kujenga Kariakoo nyingine eneo la Mbezi Mwisho

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Niliwahi kushauri na ninaendelea kuishauri Serikali kupitia Mkoa wa Dar es Salaam kuwa, wajenge Kariakoo nyingine eneo la Mbezi mwisho karibu na stendi ya Magufuli au karibu na hapo.

Nilisha eleza faida sina haja ya kurudia, huu utakuwa ni mpango wa miaka 100 ijayo.

Walio plan Kariakoo iliyopo hivi sasa ilikuwa ni mipango ya miaka 100 tangu wakati huo ambayo hivi sasa imeshapita, wakati huu miundombinu iliyopo haiwezi kuhimili ongezeko la watu.

Hivyo kuna haja ya kuja na plan B ya kujenga Kariakoo [business hub] nyingine eneo la Mbezi ambayo itaduma zaidi ya miaka 100.

Wizara ya mipango inahusika hapa.

Nilitoa maoni haya kabla ya janga la kuporomoka kwa gorofa hapo kkoo na kupoteza watanzania wenzetu 16, wapumzike kwa amani.
Kufuatia janga hilo tumeona jinsi lilivyo athiri uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, hivyo hatuna budi tukaanza kujenga kkoo nyingine eneo la Mbezi magufuli.
 
Masoko yanajitengeneza yenyewe Mkuu,

Kariakoo haijajengwa na serikali..

Mambo ya serikal kutengeneza masoko is so outdated and old school....

Washable hizo pesa zijenge miundombinu ya usafirishaji, hospital na kuendeleza majiji mengine
 
Back
Top Bottom