Ushauri kununua kiwanja Kaole, Bagamoyo

Ushauri kununua kiwanja Kaole, Bagamoyo

Oroyal

Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
90
Reaction score
88
Habari zenu wadau.Kuna kiwanja nataka kukinunua Bagamoyo Kaole naombeni ushauri wenu.Sqm 1000 sh million 12 ni karibu na beach (500metres from the beach).

Plan yangu ni baadae kujenga vi apartments hata vinne vidogo kwa ajili ya watalii wanaokuja kuvipangisha.Lakini pia nina option ya Kiromo (kiwanja kiko 5km kutoka barabara ya lami). Na hapa Kiromo bei ni nafuu zaidi maana sqm 1000 ni million 5.

Kiromo bado haijaendelea lakini mpango wangu hapo ni baada ya miaka mitano maybe ndo nijenge hapo.Sasa hapo kiromo itakuwa nyumba za kupangisha tu za kawaid sio kama mradi ninaouwazia wa Kaole.

Naombeni ushauri ninunue wapi....Kaole au Kiromo?na kwanini....na mniambie kama hapo Kaole upepp wa utalii unaleta need ya hivyo vi apartments.Nisije nikawa napanga mahesabu hewa
 
nunua kaole mkuu niunge mm ninunue kiromo,maisha ni kusaidiana
 
nunua kaole mkuu niunge mm ninunue kiromo,maisha ni kusaidiana
Unauza kaole ?kiwanja kimepimwa boss?unauzaje na kina ukubwa gani?kaole karibu na beach au ?Afu umenishauri kwa ajili ya mahitaji yako binafsi sio ?Maana sasa wewe kwanini unataka kutoka kaole kwenda kiromo?
 
Uwe muangalifu na matapeli mkuu. Bagamoyo hasa maeneo ya Kilomo, Zinga, Pande, Fukayose, Kidomole na kwengine unatapeliwa mchana kweupee tena mbele ya serikali za mtaa/vijiji.

Sina hakika na huko Kaole na hasa kama eneo husika lina title deed, labda inaweza ikawa rahisi kufatilia na kuhakiki.

Lakini kwa kiwanja cha beach chenye mita za mraba 1000 kwa 12mil jiridhishe mara mbilimbili uhalali wa muuzaji, uhalali wa hati na usahihi wa hati kama document hiyo ni ya mahali husika
 
Mkuu hata vilivyopimwa vina utapeli?Nataka kununua kwa hawa weny vikampuni vya kuuza viwanja instagrama kama abc,lado property nk.Sio kwa mtu binafsi .Na hao pia wana upigaji boss?Viwanja vilivyopimwa vya miradi ya kampuni navyo vina upigaji mkuu?Nisaidie hapo tafadhali.Kuhusu cha beach amesema kiko kaole .Metre 500 from beach.Sqm moja ni 12000
 
Viwanja vilivyopimwa ni rahisi kufanya uhakiki. Tena kama vinauzwa na hizo kampuni za upimaji uhakika unaongezeka. Inamaana hapo ni kama hati hazijatolewa kwa maana ya kwamba unapolipia ndipo hati inakua processed ili ikitoka iwe kwa jina lako wewe ukiwa ndio mmiliki wa kwanza

Hata kama utakua unanua kwa mtu(kumvua mtu) eneo lenye hati ni lina uhakika zaidi. Muhimu jiridhishe kama hati ni genuine na sio fake, mmiliki/muuzaji ni mwenyewe na sio magumashi na hakikisha spouse wake(mke au mume ana sign mkataba wa mauziano)
 
Fanya utafiti wa kina watu wanatapeliwa sana hasa viwanja potential kama hvyo
 
Mkuu hapo bagamoyo hasa marneo ya kilomo viwanja vingi vinatangazwa na mkugenzi kwa hiyo nakushauli nenda ofisi za halmashauri hapo bagamoyo kitengo cha ardhi watakupa muongozo na pia kukwepa utapeli mana bagamoyo ukizubaa unalizwa.

Hapo kilomo nimeisha 2 years na nimehama mwaka Jana, kuna jamaa alikuwa anawauzia watu viwanja na kuandikishia serikali za mitaa kumbe hapo maeneo ni sehemu ilitengwa kupitisha miradi ya serikali jamaa ikala kwao.
 
Barikiwa sana mkuu.Nimefanya hii yako ya kununulia kweny kampuni iliyoingia ubia na halmashauri.
 
Back
Top Bottom