USHAURI: Kuwa mkavu wakati wa tendo la ndoa

USHAURI: Kuwa mkavu wakati wa tendo la ndoa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
TATIZO LA KUTOPATA RAHA WAKATI WA TENDO LA NDOA

Wapo ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata raha, husikia maumivu, mwanaume katika uume lakini ni mara chache sana kulinganisha na wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili.

Mwanamke anaweza kukosa raha kabisa na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni ukeni au kwa ndani zaidi. Maumivu haya pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni maumivu wakati wa tendo ambayo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya tendo.

Kuumia wakati wa tendo
Maumivu haya hutokea pale uume unapoanza kuingia ukeni na hutokana na uke kuwa mkavu.
Hili linaweza kusababishwa na maandalizi duni kabla ya tendo, matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko na hamu ya tendo.

Kubana kwa misuli ya uke pia huchangia ingawa tatizo hili zaidi ni la kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo.
Kuwa na makovu ukeni kutokana na athari za kukeketwa, uwepo wa michubuko na vidonda au

Maambukizi ukeni mfano fangasi ya muda mrefu na maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono. Uvimbe ukeni au uwepo wa jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia ya kawaida endapo hukupona vizuri.

Kuhisi maumivu baada ya tendo
Maumivu haya hutokea muda mfupi baada ya tendo la ndoa. Mwanamke huhisi maumivu kwa ndani zaidi ukeni au chini ya tumbo. Maumivu huwa makali na huchukua muda mrefu. Maumivu ya chini na ndani zaidi ukeni huleta hisia kama muwasho mkali wa pilipili au kama unakatwakatwa na viwembe na ukinawa unazidi kupata maumivu.

Maumivu ya ndani zaidi ukeni wakati mwingine huambatana na hali ya kuhisi kama kuna kitu kinasukumwa wakati wa tendo na unapomaliza tendo ukinawa unahisi kitu kimevimba ndani ukeni kama kigololi. Maumivu huwa chini ya tumbo na wakati mwingine husambaa kulia na kushoto ya mirija. Wengine huumwa na kiuno hata kutembea inakuwa shida mara tu baada ya kumaliza tendo.

Hali ikiwa mbaya mwanamke hutokwa na damu baada ya tendo, hali ambayo siyo dalili nzuri kwani hata saratani ya shingo ya uzazi nayo huonyesha dalili hii ya damu.

Hali ya maumivu pia huambatana na kutokwa na majimaji ukeni wakati mwingine yakiambatana na muwasho mkali na harufu. Hata wanaume wanaweza kutokwa na damu baada ya tendo badala ya manii.

Nini cha kufanya?
Tatizo hili ni kubwa na lina vyanzo vingi kama tulivyoona, hivyo ni vema kufanya uchunguzi kujua chanzo halisi ndiyo tiba ifuate.

Epuka kutumia dawa bila ya kujua chanzo halisi.
Uchunguzi hufanyika katika hospitali za mikoa, wilaya kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama.
Ni vema uwahi hospitali.



 
MziziMkavu,

Nina maswali
1. Mwanamke aliyezaa miaka 3 bado anahusika na hiyo hoja yakutopona baada yakujifungua?
2. Kwa wale ambao hawaja keketwa,hana kovu, wala infection yoyote afanyeje?
3. Walio na makovu ya athari za ukeketaji hilo kovu ina maana haliponi maisha yote na wafanyeje hawa ili waweze furahia tendo la ndoa
 
Nitafute nikupe mafuta maalum kwa kazi hiyo yanayozidi hata yale ya ky. kwa ukavu wako huo kupata infection ni asilimia kubwa sana.
 
Mmh madaktar wa siku hizi hadi akushuhudie ukinywa dawa ni shida

Duuuh. Kwani ni vibaya Dr akikushuhudia? Mficha uchi....

Mwanamke kuwa mkavu wakati wa tendo la ndoa kunasababishwa na mambo mengi, kama vile kutokua na hamu ya tendo, uoga/hofu ya kufanywa, matatizo ya homoni, n.k vipi hilo tatizo limeanza lini na una umri gani?
 
Watu mnatiririiika, kwani kaandika nini? Mara ooh mwandae, ooh sijui nini, sasa Mwajuma amwandae nani[emoji15] [emoji15] Mmevurugwa bila shaka[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Back
Top Bottom