Ushauri kwa atakayesingiziwa kesi na mtu yeyote na polisi

Nazareti

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2016
Posts
413
Reaction score
443
Nimekaa kutafkari kwa kina sana kuhusu watu kufungwa kwa kesi zisizo halali, nimegundua kuwa huwa watetewa na wanasheria wasio na uelewa wa sheria ni nini na nini ni sheria.

Kwa wanasheria wa Tz, Lissu ameonekana kuwa mwanasheria bora wa Tz kwa sasa; hilo pia lilijitokeza kwenye bunge lililopita pale sakata la escrow lilipokuwa limepamba moto bungeni na hivyo kupelekea bunge kuendelea hadi usiku kitu ambacho si cha kawaida kutokea. Kwenye sakata hili wabunge wote hasa wa chama tawala walionekana hawana msaada wa kisheria hata kwa Anne Makinda Spika.

Ilipofikia hatua za kisheria na ni nini kifanyike kisheria kuhusu sakata hilo, mjadala mzima ulitawaliwa hasa na Spika, AG na Lissu. Spika makinda aligundua kabisa kuwa Lissu ni mwanasheria bora na mwenye ufahamu mwingi wa kisheria, licha ya yeye kuwa mpinzani bado hilo halikumzuia Spika Makinda kumtumia Lissu na alimpa nafasi mara nyingi kuliko hata AG.

Sasa nishauri tu kuwa ukipachikiwa kajikesi wewe mtafute tu Lissu, yaani siku hizi hata police na mawakili wa serikali wakisikia kesi inahusu Lissu, lo!hutamani wabadirishe zamu la sivyo hiyo kes ipangiwe tarehe nyingine tena ya mbali angalau wapumue. Isingekuwa ubaguzi wa kichama; Lissu alifaa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, yaani kuishinda serikali mahakamani ingekuwa kazi ngumu mno, wote wanaoshitakiwa na serikali wote wangeingia jela tu au kulipa tofauti na ilivyosasa ambapo tunategemea mda si mrefu walioshitakiwa na serikali wote watashinda na kuachiwa huru huku mawakili wa serikali wakivuta mpunga tu monthly salary na hakuna kesi waliyoshinda.
 
nadhani utamaduni unaoendelea kujengeka wa kuwa kebehi/kuwadharau wanasheria na waendesha mashtaka waserikali sio mzuri na ni wakukemewa.
state attorneys and prosecutors wanafanya kazi nzuri pamoja na changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao and by the way kushindwa kesi haimaanishi kwamba mwanasheria ni mbumbumbu au hajui sheria bali kila mwenye busara na uelewa wa sheria husema haki imetendeka
 
... Siku zote mchezaji bora huonekana uwanjani kwa chenga zake na goli anazopachika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…