Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Kudai uraia pacha ni kama kudai katiba mpya haiwezekani
 

Kamanda, unaongea point....Ubarikiwe!
 

Uraia pacha ni muhimu mno kamanda....utakuja kuyaona matunda yake....kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.


Kamanda, hao sio wajinga waruhusu uraia pacha, wameona ina faida mno na ndio maana nchi zao zimeendelea....
 

Huu ni ubinafsi na roho mbaya....nchi zilizoruhusu uraia pacha sio wajinga, na ndio maana wanaendelea, wewe utabaki na kaubinafsi kako.....
 

Uchangiaji wko umekaa kisiasa sana , naeza pata maelezo ni magabacholi wa wap na lin wamekuja kula mema ya nchi yetu chini ya baraka za watunga sheria zetu ? ( Proof ; reference ) @ hatutaki story zavijiweni
 
Uchangiaji wko umekaa kisiasa sana , naeza pata maelezo ni magabacholi wa wap na lin wamekuja kula mema ya nchi yetu chini ya baraka za watunga sheria zetu ? ( Proof ; reference ) @ hatutaki story zavijiweni
Nenda kwenye mitaa ya Dar na miji mingi uone hawa wabaguzi wambao pamoja na kuletwa na wakoloni kutunyonya walikataa kuchanganyikana nasi. Hili halihitaji utafiti wala kujificha nyuma ya siasa. Magabacholi wapo wengi tu. Napenda sana kutumia jina la magabacholi hasa nikizingatia wanavyowabagua waswahili wenzetu waitwao Jarawa kwenye visiwa vya Andaman ambao wanawatumia kama wanyama kufanya utalii.
 
Ikumbukwe kuendelea kwa mtu au taifa kuna factors nyingi sana zinazohusika.
Kuna nchi nyingi duniani zimeendelea sana kwa kutumia raslimali zilizopo nchini mwao,vipi hapa kwetu,raslimali zimetutoa?
au napo tunakwamishwa na kutokuwa na uraia pacha?
Mimi naona kwanza tuwekeze kwenye kuwa na mioyo ya kizalendo tukifanikiwa ndo tuingie huko kwenye upacha.
 
Huyu Malamula ameanza kuni-disappoint sana. Ilikuwaje akapewa hii nafasi?
 
Huyu Malamula ameanza kuni-disappoint sana. Ilikuwaje akapewa hii nafasi?
Wewe ni wale wenye roho ya korosho ambao walishindwa kwenda majuu na kuwaonea wivu wenzao kiasi cha kuwawekea pini kwa sababu tu ya roho mbaya na ujinga au?
 



Tanzania iko tofauti na hizo nchi na mifano yote hiyo.Tatizo nchi yako hauijui ndio maana unalalamika


Haitakuja kutoka in your lifetime na Mulamula hauwezi

Unazungumza 85% wasiotaja vs 0.2% wanaotaka...usiulize najuaje


Kuna mengi ya kufanyia kazi kuanzia umaskini na sio uraia pacha

usipoteze muda humu, it will nevee happen TZ
 
Mheshimiwa Malamula sijui kama ni Raia Pacha, namsihi aanze taratibu.

URAIA PACHA SI WA KUCHAGUA, NI WA KURUHUSIWA NA NCHI YA PILI KWA MASHARTI YAO. Kabla hujapewa uraia pacha wa USA, ni lazima ule kiapo kifuatacho, hadharani:

Full Oath of Allegiance to the United States

“I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America against all enemies, foreign and domestic; that I will bear true faith and allegiance to the same; that I will bear arms on behalf of the United States when required by the law; that I will perform noncombatant service in the Armed Forces of the United States when required by the law; that I will perform work of national importance under civilian direction when required by the law; and that I take this obligation freely, without any mental reservation or purpose of evasion; so help me God.”

Hii ni ya USA, kuna ya Israel, Ujerumani, India, nk. Kwa ufupi, hakuna nchi inayokupa Uraia wake kama wewe ni Raia wa nchi ingine. Tumepewa mifano ya South Africa (apartheid), Kenya (Mungiki, maumau), Rwanda (Genocide), Ethiopia (Dergue), hizi si nchi za kulinganusha nazo.

Tumeambiwa mashoga na mafisadi na majambazi na malaya eti tunao wengi si raia pacha. Hawa wapo kila mahali, mambo yao hayahusiki.

Mheshimiwa Balizi: hiyo ramani ya AFRICA ni ya nchi ZINAZOOMBA uraia pacha: naomba nipe ramani ya nchi ZINAZOOMBWA na KURUHUSU uraia pacha, nchi za EU, USA, JAPAN, INDIA, ISRAEL, AUSTRALIA, RUSSUA, CHINA.
 
Mheshimiwa Balizi: hiyo ramani ya AFRICA ni ya nchi ZINAZOOMBA uraia pacha: naomba nipe ramani ya nchi ZINAZOOMBWA na KURUHUSU uraia pacha, nchi za EU, USA, JAPAN, INDIA, ISRAEL, AUSTRALIA, RUSSUA, CHINA.
Unaelewa urataibu wa uraia pacha kweli? Nchi zinaomba uraia pacha kwa nani? Na nchi zinaombwa uraia pacha na nani?

Siku zote nimesema, wengi wanaobisha juu ya suala la uraia pacha hawajui hata utaratibu wa uraia pacha ukoje.

Kwani nani amesema ncho zote zinazoruhusu uraia pacha zinashurutishwa na kiapo cha uraia cha Marekani? Na sisi Tanzania tukiweka kiapo kama cha Marekani, so what? Acha Wamarekani wao ndio wawakatalie Watanzania kuoma uraia wa Marekani kwa ajili ya sisi kuwa na kiapo kama chao. Hakuna sheria Marekani inasema huwezi kuomba uraia wa Marekani kwa kuwa kiapo cha nchi yako kiko sawa na cha Marekani
 
Unazungumza 85% wasiotaja vs 0.2% wanaotaka...usiulize najuaje
Inawezekana hao 85% wasiotaka ni vihiyo kama wewe, ndio maana tulikubali mfumo wa vyama vingi japokuwa 80% walipinga. Tukipoiga kura ya kukubali au kukataa chanjo ya Korona, inawezekana wajinga wakawa wengi zaidi upande fulani. usiokubalika na werevu. Tunaijua nchi yetu, ina tatizo la ujinga, umasikini na maradhi, sasa lazima tukumbuke kuwa wajinga nao huwa wana uhuru wa kutoa maoni yao ya kijinga, lakini sio lazima tuwasikilize.
 
Wewe ni wale wenye roho ya korosho ambao walishindwa kwenda majuu na kuwaonea wivu wenzao kiasi cha kuwawekea pini kwa sababu tu ya roho mbaya na ujinga au?
I say, hadi leo kuna watu wanaabudu kwenda majuu!!! Pole sana Mkuu. Umechelewa sana.
 
I concur 200%. I am one of the affected and i hate the fact that when i come to Tanzania to visit i am taken as a foreigner (this thing hurts) why because i couldn’t keep both nationalities. I love my country alot and i wanna do alot but my hands are tight cuz at the end of the day i am just a “foreigner”. Born, raised and grew up in Tanzania, now i am a foreigner. Most countries surrounding us allow dual citizenship, it’s high time Tanzania grew out of old mindset and be open minded, that way investors will even feel okay to come. That’s all. Until then i will hope and pray.
 
Jamani, uraia pacha hauuzwi, labda kama nchi iamue tuwe na utaratibu wa kuuza uraia pacha. Kwa hiyo Mchina hawezi kuja Tanzania kununua uraia pacha.

Kigezo cha kwanza cha kuwa raia pacha kwa kawaida ni kwamba huyo Mchina awe ameishi Tanzania mfululizo kwa kipindi kisichopungua miaka 5, au awe ameoa/ameolewa na Mtanzania na kuwa katika ndoa kwa zaidi ya miaka 3, nk. Hivyo ni vigezo tutaamua wenyewe, hakuna mtu wa kutupangia. Tunaweza hata kuwa na sharti kwamba Mtanzania mwenye uraia pacha asigombee nafasi ya kisiasa kama ubunge na uraisi, au asitumike katika nafasi za vyombo vya usalama kama JW, TISS na polisi. Ni uamuzi wetu.

Kwa hiyo uraia pacha hautolewi kama kununua nyanya sokoni, unakuja kwa masharti ambayo kila nchi inaweka.

Ni kweli kuna nchi zimeweka masharti kwamba ukiingiza nchini kuanzia USD 250,000 una qualify kupewa uraia. Na nchi kama Norway wakati fulani ilikuwa ukioa au kuolewa na Mnorway basi unakuwa raia wa Norway moja kwa moja, wakaja wakabadilisha kwamba lazima uishi na mkeo/mumeo kwa angalau miaka 3, na kuwe na uthibitisho kuwa kweli mnaishi kama mume na mke.

Kwa hiyo watu wengi hawaelewi suala la uraia pacha, wanadhani watu watakuja kuununua Tanzania bila vigezo. Haiko hivyo

Watu watakaopata uraia pacha kirahisi ni Watanzania wenyewe, sio raia wa nje, na hao Watanzania kupata uraia pacha na nchi nyingine inategemea masharti ya nchi wanayotaka kuchukua uraia wa pili
 
I say, hadi leo kuna watu wanaabudu kwenda majuu!!! Pole sana Mkuu. Umechelewa sana.
Siyo kuabudu wala nini. Acha vijana wenzako walioweza kwenda kule wapate haki yako badala ya roho ya korosho. Majuu patabaki kuwa majuuu as long as Afrika bado tuna mijitu yenye roho zenye kutu kama wewe.
 
Kwani wahindi sasa hawachukui na hawana uraia pacha? Mkiwaendekeza watawamaliza hasa ikizingatiwa kuwa wanawatumia nyinyi manajiona wazalendo kuibia taifa. Waliokaa nje hawababaishwi na wahindi. Kwani huko nje wote wanaonekana people of colours. Wapo kwenye kapu moja katika kubaguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…