Ushauri kwa Bima ya Afya (NHIF): Wekeni uwiano mzuri kwa wanufaika wa wachangiaji wa mfuko huo

Ushauri kwa Bima ya Afya (NHIF): Wekeni uwiano mzuri kwa wanufaika wa wachangiaji wa mfuko huo

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Posts
4,635
Reaction score
2,271
Napenda kuishauri NHIF kuwa kama utaratibu unaruhusu watu sita (6) kwa mchangiaji basi aruhusiwe kuwaweka bila vipingamizi ilimradi wasizidi idadi hiyo inayokubalika.

Mfano kama mchangiaji hana watoto wanne aruhusiwe kuwaweka wengine bila kikwazo. Kama mchangiaji hana wazazi wote au mmoja halikadhalika aruhusiwe kujaza nafasi hizo.

Pia kama mchangiaji hana Mke au Mme basi aruhusiwe kujaza nafasi hiyo. Ni ushauri wangu kwenu NHIF naamini itahamasisha zaidi wachangiaji na kuipenda NHIF. Nawasilisha.
 
Na sie tunaokaa na wamama bila kufunga ndoa imekaaje hii kwenye bima ya familia ya watoto wa familua hii?
 
Back
Top Bottom