Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

....ondoa hiyo 'kama'.,sema mtashikilia msimamo wenu!..
..si huwaga mnajinasibu hata Mandela alikaa jela zaidi ya miongo miwili,nendeni sasa to that extreme end KAMA kweli mna dhamira ya dhati ya ukombozi kwa wananchi maskini!
....tena na nyie viongozi viongozi muwe frontline.,sio mnatoa matamko tu huku nyie mnapigwa na viyoyozi!
 
Magufuli dikteta anayependwa na walalahoi, anachukiwa na mafisadi.

Naona huyu dikteta ana nguvu kubwa nyuma yake, nguvu ya walalahoi ni ngumu kuivunja. Mumuache tu dikteta Magufuli afanye udikteta wake mpaka pale walalahoi watapofungua milango ya nyumba zao na kusema, tumechoka utawala wa kidikteta.
 
Huu ndio wakati hasa wa CHADEMA kuionyesha dunia kuwa wao ndio chama kikuu cha upinzani Tanzania vyenginevyo wakishindwa tena huu mtihani uliopo mbele yao watakosa sifa zote za Kuwaita wao chama kikuu cha upinzani.

Niwakati muufaka wa wao kuidhihirisha kwa vitendo slogan yao ya "PEOPLE'S POWER" na waondokane na kuitamka kwa maneno tu.

Hali kama hii ya siasa iliwahi kutokezea wakati wa Mh. Mkapa baada ya uchaguzi mkuu wa 2000 pale alipozuia harakati zote za kisiasa kwa wapinzani ili aachiwe yeye na serikali yake watekeleze ilani yao.

Kwa wakati huo CUF ndio iliyokuwa chama kikuu cha upinzani hawakuikubali hii hali na ikapelekea kuja na slogan ya "JINO KWA JINO" kama ishara ya Kapinga ukandamizaji wa CCM na serikali yake.

CUF kupitia kiongozi wao SHUPAVU Professor Lipumba wakaipinga hii hali kwa maandamano ya lazima ambayo yanaruhusiwa kikatiba.

Pamoja na Mh. Mkapa na Mahita kuyapiga marufuku kwa nguvu zao zote CUF kupitia wanachama wao shupavu waliandamana na wengi wao wakauliwa, wakajeruhiwa na kupata ulemavu wa kudumu lakini walifanikiwa kuiondoa hali iliyokuwepo na siasa zikarudi kama kawaida kwa wapinzani.
 
Pasco acha hahari zako wengine tunahamu ya kuvunja watu wewe unaleta sanaa za kuwapa ushauri sisi tutapata wapi watu wa kupiga? Acha waje tufanye kazi yetu tupate posho za kazi ya kutukuka.
 
Unadhani Magufuli kama Lowasa? Sasa jaribuni muone moto wake.
 
Pasco bado kidogo sana utang'olewa kucha au meno au vyote kwa pamoja, tena bila ganzi.
Unathubutu kumwita DICTACTOR mheshimiwa mtukufu sana rais ambaye hatakiwi kukosolewa na mtu yeyote! mark my words.
 


Pasco kuna tofauti kati ya kuandamana na kufanya mikutano. CHADEMA wamedhamiria kufamya mikutano na sio kuandamana!
 
Pasco nadhani elimu yako inatosha Ila ushauri kwa CHADEMA waambie waliokutuma pamoja na ngosha mwenzio pelekeni maziwa makuu inaeleweka
 
Unajua kwa tanzania elimu ya siasa na uraia kuna mapungufu sana........
Kiukweli wapinzani pamoja na serikali wote wanamaeneo wanakosea pia wanapatia.........
Nikianza na wapinzani........hawa mlengo wa hoja zao zimekaa kukosoa serikali sio kwa lengo la kuijenga bali kuiharibia ili nao wapate ridhaa ya wananchi katika kuliongoza taifa.....hili si jambo zuri hata kidogo.......huu ni usanii kabisa....

Nitawapa mfano wa inshu ya sukari.........wabunge wengi wa upinzani walichachamaa sana kwa kuwaambia wananchi kuwa serikali haiwatakii mema kwa kuzia uagizaji wa sukari usio fuata taratibu za kisheria za biashara katika manunuzi........nakumbuka walituhadaa wananchi kuwa sukari haitokuja kushuka maana serikali inakosea......leo hapa mimi nipo kilimanjaro nimetoka kununua sukari kilo 1800. Tokea ilipokuwa 3000. Sasa najiuliza huwa wapinzani wakiongea wanatumia taarifa za wapi.......maana ni kama wanapotosha uma.........mimi naona ni kama wanaweka jitihada nyingi kubeza jitihada zinazofanywa na kupotosha uma wa watanzania.......na asilimia kubwa ya watanzania si wafuatiliahi huwa wanajiridhisha na story za kusadikika ama za mtaani au post za facebook ambazo huwa wanaozipost hawajulikani ni akina nani plus wanamalengo gani.......

Swala la elimu......wanabeza sana maamuzi ya kuweka vigezo ambavyo vitarejesha thamani ya elimu sio kama sasa kila mtu anadegree uchwara halafu uwezo zero kazi kupiga domo tu.....wapinzani wanakazana kuropoka tu ili wapate hii popularity kama ya akina wema na diamond kwa kuropoka.......

Me nasema mh.raisi yupo sahihi kukataza hizi kelele zisizo na tija yeyote ........hawa wapinzani si muda wote.wapo sahihi......wanayohaki ya kuikanya......kuirekebisha na kuikosoa serikali.......ila sio kwa staili hii wanavyofanya ya kuibeza na kuikejeli badala ya kuishauri.............wapinzani hawaongei jipya kazi yao ni kubeza .Unapomkosoa mtu......toa suggestion ......au wazo mbadala ila sio unangojea mwenzako akosee ndipo povu likutoke........tena unatoa kauli za kuhatarisha amani na usalama wa raia........

serikali ni kweli inakosea kuwazuia wapinzani kuongea na uma lakini ni kwasababu wamegundua mnaitumia fursa hiyo kuongea vijembe.....na kukejeli serikali ndio maana wanawabana kwa kila namna .......hata ningekuwa mimi nisingeruhusu mtu ambaye hauna ridhaa ya kuendesha nchi uongee maneno ya uchochezi badala ya kutoa ushauri.......hii kitu alishaifanyaga mbatia mara moja tu......aliishauri serikali kuhusu kuhamisha maofisi yao maeneo ya posta na kuyasambaza maeneo mengine ili kupunguza msongamano wa foleni za magari asubuhi watu wanapokwenda makazini maana msongamano huu unaitia serikali hasara kila siku ya mabilioni......na ndio maana kikwete akamkubali sana akampa nafasi ubunge viti maalumu.........mrema huyo hapo amepewa nafasi anashirikiana na serikali......huo ndio upinzani wa ukweli unatakiwa kuwa sio hawa wakina zitto wanakwenda kusoma vitabu na notes za shule wanakuja kutuletea theory za utabiri hapa.....wanaboa sana......
 
Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.

He should be careful of what he wish for!

Hii kauli inaqualify kuitwa mkakati wa uhaini.

Rais aliyechaguliwa kikatiba hakuna njia isiyo ya kihaini ya kumtoa madaraka kabla ya uchaguzi.
 
Watch out.. Mnataka ku over through the government... Watanzania wazalendo tumempa kura Magufuli na tunamwamini.. Nyie subirini 2020 muonekano anavoshinda kwa kishindo.. Watanzania wana akili na niwaelewa msidhani mashabiki wa ukawa bado mpo Milion 6..mmepungua sana mpo million 3
 

Ajaribu kufanya
The world is watching......na Tanzania ni sawa na tone la maji katikati ya maji ya bahari!!
I hope, umenipata.....
 
Unadhani magufuli mjinga kama Lowasa? Sasa jaribuni muone moto wake.

Mbona nyinyi WAGALATIA huwa hamna hekima ya kuheshimu wakubwa ambao wanaweza wakawa na umri sawa sawa na wazazi wenu!!!????

Hivi akitokezea mtu akamwita baba au mama yako "MJINGA" wewe utaridhika na hiyo hali!!??? Kama haoutoridhika basi vivyo hivyo watoto wa Mh. Lowassa hawafurahii kuona baba yao anatukanwa hivyo.

Mimi nadhani CCM wengi wenu ni wanawaharamu maana hii tabia yako ndio tabia ya wanachama na wapenzi wengi wa CCM.

Ukienda Zanzibar wako watu kama wewe ambao tabia zenu mnafanana "AKINA SHAKA HAMDU, BORAFYA NA MAREHEMU ASHA BAKARI"

hivi haitoshi kupingana na mpinzani wako kwa maneno na vitendo vya heshima!!!!!!???????????

JIFUNDISHE KUWEKA AKIBA.
 

KAMA CCM wanajiamini kuwa wananchi wanawapenda basi waweke tume huru za uchaguzi na waruhusu katiba ya warioba ipigiwe Kura.

Vyenginevyo wanajitekenya na kucheka wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…