Ushauri kwa CHADEMA kuhusu siasa mtandaoni

Ushauri kwa CHADEMA kuhusu siasa mtandaoni

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Niende moja kwa moja, nawashauri chadema mkitaka kufanikiwa, wekezeni sana kwenye mitandao ya kijamii, ajirini watu kabisa ikiwezekana.

1. Israel na Hamas vita yao kubwa ilikuwa ardhini, lakini vita kbuwa zaidi ilikuwa mitandaoni. waliajiri watu kabisa ambao akiamka asubuhi hadi jioni anaenda kazini kwa ajili ya kuongea mambo in favour of their position.

2. Israel amefanikiwa sana kwa sababu walifanikiwa kurusha matukio mengi ya vita hata kwa simu tu, na Hamas walifanikiwa zaidi kwa kurusha namna raia wanavouawa ili dunia ijue.

3. Hamas walifanikiwa zaidi kusambaza kwa njia ya mitandao mambo yanayoendelea jambo lililowafanya kupata sapoti ya watu ulaya na marekani nzima, vyuo vikuu hadi makazini watu walikuwa wanasapoti hamas why? kwa sababu ya nguvu ya mitandao.

4. mkitegemea hizi tv kama ITV jana iliyokuwa inakatikakatika, mtaambulia mabua. katenikateni clip ndogo ndogo ambazo raia wa kawaida hatapoteza bando kubwa, watu watarushiana kwenye whatsapp na mitandao mingine na hiyo ina nguvu kuliko hata television.

hata hii changiachangia ambayo wengi lazima tunachangia, pelekeni mitandaoni zaidi, digital employees wenu wafanye kazi ya ziada sio kujibu na kutukana watu ila kuelewesha kwa uvumilivu na kubadilisha mioyo ya watu wanaoamin ccm ni kitu.
 
Back
Top Bottom