Elections 2010 Ushauri kwa Dk Slaa

Nani atamsikiliza!.Ndio maana nikamtaka asafiri akazungumze na Seif.
Nyinyi hamna jema mutakalomfanyia dkt.Slaa,mbali na kumuongezea machungu.

Siasa za majitaka, Siasa za kuogopa vivuli vyenu, Siasa za kuganga njaa na zaidi ni Siasa za kuukubali Ubwana na Utwana katika nchi mliyopewa na Muumba wenu.
CHAKE CHAKE CHANGU CHAKE. KWao siku zote ni kwao, mnajikomba kwa kila hali hata kumwaga damu za ndugu zenu ile kwenu kuwe kwao.
Hii ni AIBU yetu wote.
Tumewavumilia kwa muda mrefu sana, sasa tunageuza meza.

Nguzo kuu ya Siasa za akina AMI ni Mashirika Makubwa ya Kimataifa ambayo ni mbadala wa serikali za kikoloni yanayotumia ujinga ule ule wa Karl Peters wa Kuwahonga Watawala wetu Shanga za Viunoni ili Wakoloni wale wale kwa kutumia Multinational Cooperation waendelee kunajisi nchi yetu vile wapendavyo.
Leo hii wajomba zako pale Ikulu wanapewa shanga za viunoni kwa umbo la vijisenti na kuzipeleka huko Jersey ,Dubai,S.Afrika na Mabenki mengine ya kigeni ili wapate wanunulia wake na Mabinti zao Gagulo za bei mbaya pia Magari ya Kifahari yatembeayo katika Barabara duni zenye mashimo, foleni ndefu na vumbi.

Dr Slaa doesn ot take NEC's NO for an Answer so do we.
 
Mawazo ya wana JF wengi waliochangia hapa inaonesha wana mawazo ya kwenda kushitaki Ulaya juu ya kushindwa kwao.Kwani wao hawajasikia kwamba Tanzania kumefanyika uchaguzi na dkt.Slaa hajaridhika na matokeo?.Hata Seif pia aliamini kushtaki,akafanya hivyo mpaka akachoka.
Wamesikia kuhusu uchaguzi wa Myamar na kutoa tamko.Obama mbona hajasema kuhusu uchaguzi wa Tanzania lakini tayari katoa tamko kuhusu Myamar.
 
We Ami ni mpuuzi tu, kama unasema Dr Slaa hajakomaa kisiasa je Makamba ndo kamomaa???? Au Chenge mzee wa vijisenti na akina lowasa ndo wamekomaa??? Nchi hii wameisaidia nini???

Dr Slaa ameisadidia sana Tanzania yetu kwa kufichua wizi mkubwa je Kikwete wako kaisaidia nini nchi?? Kama siyo kula pesa za wananchi halafu anakwenda kubembea jamaica???
 

Mbona balaa la kenya marekani aliingilia kati?? Wewe usijifanye unajua sana mambo haya......Marekani anajali maslahi yake pale anapoona yata hatarishwa, sasa Tanzania kuna fujo gani mpaka apige kelele wakati anaona hali ya nchi bado ni shwari??
 
Mbona balaa la kenya marekani aliingilia kati?? Wewe usijifanye unajua sana mambo haya......Marekani anajali maslahi yake pale anapoona yata hatarishwa, sasa Tanzania kuna fujo gani mpaka apige kelele wakati anaona hali ya nchi bado ni shwari??
Kumbe hali ni shwari!,basi ina maana uchaguzi ulikwenda vyema.Sasa ya nini kulalamika.Na huko Myamar nako mbona Marekani imeshatoa tamko hata matokeo hayajatoka.
Mimi sijifanyi kuyajuwa sana haya mambo ila nakuomba na wewe uyasome kwanza.
Huko Azerbajan mambo ni hivi:
In Azerbaijan, the ruling party is predicting victory after Sunday's presidential election. The opposition is claiming the ballot has been rigged.Final results are expected later on Monday.

Na huko Afghanistan ni hivyo hivyo:
Dissatisfaction is mounting in Afghanistan over the parliamentary elections held in September.
Many candidates who took part claim there was widespread fraud and vote-rigging. And as Al Jazeera's Sue Turton reports from Kabul, the Afghan capital, they are taking to the streets to make their voices heard.
 
Nguvu ya mnyonge ni kelele na haki huja kwa kuitafuta
huwezi kukaa kama boga ukitegemea kuipata haki
hatuwezi kuruhusu hali ya kuiba kura iendelee na kukubali uvumilivu.
 
Na ushauri huu ni crap
 
angalia kwenye red na green:wewe ni kibaraka.uwezo wa slaa huwezi kulinganisha na mtu yeyote kati ya wagombea wote wa mwaka huu,tuna marais 2 kwa sasa,slaa kipenzi cha wananchi na wapenda mabadiliko na kikwete rais wa kuchakachuliwa

I like that, no wonder sherehe za kuapishwa zilitawaliwa na green na Yellow. Ingekuwa Dr Slaa naamini pasingetosha
 
Tukiwa na mawazo rahisi kama AMI kweli maendeleo hayatakuja! Yaani usikie mtu katembea na Mkeo umuache hivihivi tu hata kumshtaki kidogo ushindwe!!!!!!!!!!!!!!!!?
 
akili zako finyu, soma vitabu uelimike. anza na 'stop worrying and start living'
 
Ninachokiona ni kuwa Ami asilaumiwe hata kidogo,huenda amekulia kwenye ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI WA CHAMA.Enzi za mtu kuwekwa na kivuli halafu unaambiwa upige kura ya ndio au hapana.Hivyo mawazo haya yanahitaji yayeyushwe kwanza maana ana mawazo ya woga,ya kukubali kila haki yake inapochukuliwa anasema ndio mzee.Jifunze kwa waliopigania uhuru ktk nchi mbalimbali kama walikuwa na mawazo kama yako.Jifunze kwa Mandela,Martin Luther King,Samora Machel,Patrick Lumumba,Mashahidi wa Uganda,Yesu,Mohamed S.A.W etc kama sio watu hawa leo wananchi wao wangekuwa je?Acha woga,hakuna atakayekudhuru kwa kutetea haki,hata kama watakudhuru utaacha historia yenye kumbukumbu nzuri.
Hii ni kwa ajili yetu na vizazi vinavyokuja,leo hii tunapoongelea kuhusu waliopigania haki ya watu wao kama Mangi Meli,Mkwawa,na wengineo sio kwamba walikuwa na mawazo kama yako wakaweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…