Ushauri kwa Fei Toto, fuata maslahi

Ushauri kwa Fei Toto, fuata maslahi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Hapa ulipofika ndiyo uko kwenye kilele cha taaluma yako

Umefika hapa kwa kipaji na juhudi kazako na unastahili kupata mavuno ya kazi zako.

Bahati mbaya maisha ya bongo yamejaa utapeli mwingi,

Wenzetu ulaya hatua hizi walishazipitia na wakaweka utaratibu mzuri. mchezaji anaweza kuchukuliwa akiwa wa kawaida kama ulivyochukuliwa, akapewa mkataba wa kawaida kama uliopewa.

Lakini akionyesha kiwango cha juu, timu humuita na kukaa mezani kumpandhia maslahi na kupandisha viwango vya usajili.

Tanzania matapeli wanachotazama ukicheza kwa kiwango wanawaza wao kunufaika na juhudi zako tu na wala hawawazi kubadiri mkataba ili na wewe juhudi zako zikunufaishe.

Kama azam wanakuwekea mezani milioni 16, yanga wakitaka kukubakiza ni kukupa kiasi hichohicho.

Hapa una nafasi kujadili good terms azam na mkataba mpya wenye maslahi yanga. Achana na mkoloni mweusi anayeamini mzaw hawezi kulipwa kama mgeni.

Acha kusikiliza wajinga wanaodai huwezi kulipwa kama azizi ki au mayeae, sikiliza anayekuja kukwambia kipaji chako ni kikubwa unahitaji kulipwa kiasi kikubwa, huyo ndiye rafiki kwako na ndiye msikilize.

Anayesema tofauti ni mnafiki na mkoloni na hakupendi bali kutaka kukutumia tu.
 
Hakupata mshauri mzuri. Inawezekana alipewa tita kubwa la pesa akakurupuka kuvunja mkataba kimakosa. Ndiyo maana ni lazima kila machezaji ajiwekee meneja ambaye anajua sheria za mikataba vizuri.

Njia ilikuwa ni fupi sana, yeye angekwenda Yanga na kuwaambia ana ofa hiyo awasikilize watasemaje kabla hata mambo hayajatoka nje; akishindwa kuelewana na Yanga, basi anawaambia Azam watume maombi rasmi ya kumtaka kama ambavyo FIFA inavyoagiza. Sasa Azam hawakutaka kwenda njia ya kawaida ya kufanya uhamisho au hata kumkopa wakatumia njia ya mkato ya kumrubuni eti avunje mkata awe mchezaji huru kusudi iwe rahisi kwao kumchukua.

Kama ni kweli alirubuniwa na Azam, basi hayo ni makosa kwake yeye pamoja na timu ya Azam; FIFA inaweza kuwachukulia hatua iwapo utapeli huo utatolewa ushahidi wa kutosha
 
Mwambieni kikwete atulie amuache kijana afocus katika career yake ili Apate returning
 
Hakupata mshauri mzuri. Inawezekana alipewa tita kubwa la pesa akakurupuka kuvunja mkataba kimakosa. Ndiyo maana ni lazima kila machezaji ajiwekee meneja ambaye anajua sheria za mikataba vizuri.

Njia ilikuwa ni fupi sana, yeye angekwenda Yanga na kuwaambia ana ofa hiyo awasikilize watasemaje kabla hata mambo hayajatoka nje; akishindwa kuelewana na Yanga, basi anawaambia Azam watume maombi rasmi ya kumtaka kama ambavyo FIFA inavyoagiza. Sasa Azam hawakutaka kwenda njia ya kawaida ya kufanya uhamisho au hata kumkopa wakatumia njia ya mkato ya kumrubuni eti avunje mkata awe mchezaji huru kusudi iwe rahisi kwao kumchukua.

Kama ni kweli alirubuniwa na Azam, basi hayo ni makosa kwake yeye pamoja na timu ya Azam; FIFA inaweza kuwachukulia hatua iwapo utapeli huo utatolewa ushahidi wa kutosha
Wote tunafahamu kuwa hilo unalolipendekeza ni ngumu kuwezekana kwenye hizi Club zetu hususani kwa wachezaji wazawa.

Mfano Farid Mussa leo aseme nataka mniongezee mshahara akataja ofa yake kuwapa uwanja management imfikirie unafikiri hilo litawezekana?

Halitawezekana kwasababu mchezaji hayupo kwenye competition ya kuhitajika na timu nyingine licha ya impact yake katika kuisaidia timu.

Halitawezekana kwasababu pia mchezaji hana option nyingine nje yapo kwa maana ya kwamba hata ikitokea akishindwa kufika makubaliano na management na ikaamua kuachana naye, hana sehemu nyingine ya kwenda atakayopewa hilo dau analo demand.

Na baada ya kuachwa hata akipata hiyo sehemu nyingine ya kwenda basi sio tena kwa dau lile alilokuwa analipwa Yanga inawezaa ikawa chini zaiditena katika timu ambayo ndogo itayomfanya azidi kudidimia kutokana na mchango wa wachezaji wengine kuwa ni wa uwezo wa chini.
 
Mnamjaza dogo upepo, mwisho akipotea mnaanza tena kumcheka. Katika mazingira ya kawaida kabisa, kila ajira mwajiriwa anaingia mkataba wa kisheria na mwajiri wake.

Na inapotokea mwajiriwa kama huridhishwi na mazingira yako ya kazi, au mshahara unaolipwa na mwajiri wako, kuna taratibu za kufuata.

Siyo kwa sababu Azam wanamuona Fei Toto leo kama mchezaji mahiri kwao, basi wapite tu njia ya mkato na kumchukua. Mikataba ya wachezaji haiendi hivyo! Hata wenyewe sidhani kama wanalipa wachezaji wao wote hiyo mishara ya milioni 16 kwa mwezi.

Wafuate taratibu za wazi, kama walizofanya Yanga za kuwaandikia barua ili kuwasajili wachezaji wao wawili; James Akaminko, na Kipre Junior! Kutumia njia za mkato, kwa kumrubuni mchezaji; sidhani kama itamsaidia Fei Toto katika maisha yake ya soka.
 
Back
Top Bottom