field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,732
Nimefuatilia baadhi ya hotuba za rais Magufuli, Hotuba hizo zipo "vague" na zimekosa coherent na mvuto kwa wananchi wengi isipokuwa kwa wachache walio makada wa CCM wanaojilazimisha kufurahia wakiogopa "repercussions" iwapo watafikiri tofauti au wata-"comment" lolote.
Nyingi za hotuba zake zinaongelewa aidha WANAWAKE, KUOA, KUPIGA nk. Mfano halisi ni kwenye msiba wa aliyekuwa meya/mkurugenzi wa Dar, Masaburi aliyefariki, rais akiwa kwenye msiba aliropoka kuhusu kuwafahamu wake wanne wa marehemu akiwa kwenye msiba....Nani alimwambia anapaswa kuongea kitu asichotakiwa kufanya kwenye msiba? juzi tena akiwa kwenye sherehe za kitaifa alimsema kuwa Rais mstaafu Ali H. Mwinyi ameishi muda mrefu kwa sababu ana wake wawili, Akiwa na Rais Museveni kwenye mkutano muhimu wa nchi zetu akatoa neno ambalo ni offensive kuwa " Rais Museveni aliishi Tanzania huenda ameacha watoto huku kwetu" hapo Museveni akiwa na mke wake, kwa wale walioiona hiyo "clip" utagundua kabisa hayo maneno hayakumpendeza kabisa Museveni kwa jinsi "expression" ya uso wake ulivyobadilika, hakutegemea kusikia aliyoyasema Magufuli. Ni kila mara huyu rais anaropoka mambo yanayohusiana na mahusiano na wanawake au matusi matusi tu! "mara sitafuti mke", "mara ninaowachagua watu wananiambia nina uhusiano nao", yote ya nini hayo? Mbona hasemi ya Sundi Maloto?
Siyo hayo tu juzi kwenye hotuba yake, alimsema waziri Jaffo kuwa ana wake wanne (4) Sasa hata akiwa na wake wanne inamhusu nini? Yeye si muislamu? hata hivyo ana mke mmoja tu, rais wetu anajiabisha sana.
Rais anafanya mengine mazuri lakini asijiabishe au ni utamaduni wa kule anakotoka...Paschal unaweza kutuambia?