Ushauri kwa mamlaka ya uteuzi kuhusu atakayepeperusha bendera ya CCM jimbo la Rorya

Ushauri kwa mamlaka ya uteuzi kuhusu atakayepeperusha bendera ya CCM jimbo la Rorya

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Zaidi ya wana CCM 40 wametia nia na kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa Oktoba, 2020. Mmojawapo wa watia nia na aliyechukua fomu leo ni Ndugu Lameck Okambo Airo ambaye mwaka jana alielezea umma kuwa hatagombea tena katika uchaguzi unaokuja mwaka huu.

Upande wa CHADEMA tayari wamempitisha Ndugu Wenje kuwa mgombea wao na hapa ndiyo kuna vita kali. Kwa ujumla kwa sasa Lakairo hana uungwaji mkono kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita na wengi hawampendi kwa sababu ya kutohudhuria vikao vingi vya Bunge, Kutozungumza Bungeni hata sentesi moja kwa miaka kumi katika Bunge la Jamhuri ya Tanzaniau na kutosimamia miradi mingi inayotekelezwa kwenye Jimbo hasa Barabara ya lami toka Mika mpaka Shirati.

Hivyo mamlaka ya uteuzi mliangalie suala hili hata ikibidi kutuma watu wa kufuatilia jinsi Lakairo anayokubalika katika Jimbo vinginevyo tusije tukamwachie Wenje Jimbo kwa uteuzi ambao haukufanywa kwa umaakini. Nawasilisha.
 
Twende na Prof . Julius Nyaongo, msomi mwenye maono
 
Back
Top Bottom