Ushauri kwa mdau aliyeamua kujiajiri lakini amekwama

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Mshauri mdau huyu aliyeamua kujiajiri , alipata fedha kidogo akapanga fremu na fremu haikua kwenye hali nzuri akafanya marekebisho kidogo(hela kidogo ikatumika), akanunua na samani chache kama meza na kiti, ni duka la mpesa na liko eneo zuri sana lenye watu.

Sasa hela imekata, anafanya nini? je aingie ubia na mtu mwenye mtaji wakubaliane kimaandishi kwa uwazi kabisa faida itakayokua inapatikana wagawane, au aende benki kukopa je atakopa kwa dhamana ipi sababu hana dhamana zozote ambazo benki nyingi zinahitaji kama kiwanja/nyumba/gari ..au akopeshwe na mtu( amejaribu kwa wadau mbalimbali hajafanikiwa).
 
Auze line ya mpesa hela atakayopata akanunue karanga hazikaange Azipaki fresh hauze bila kusahau clips na ubuyu .

Ni biashara zinazoitaji mtaji kidogo ila faida kibao kama anakaa sehemu yenye movement za watu.
 
Kwahio wakati anafanya huo ukarabati,ananunua samani hakujua anapunguza mtaji wake?
 
Tafuta mtu mwenye mtaji ila yeye hana eneo la biashara ,wewe utakuwa unamili eneo la biashara yeye mtaji ,so kwa makubaliano ya kugawana faida itayopatikana! Kwa style hiyo unawezakuta unarudisha pesa yako iliyotumika
 
shukran kiongozi
 
ila si ifae ukute ambaye hana sehemu basi na yeye awe na wazo sawa na biashara yenyewe husika
 
Kwahio wakati anafanya huo ukarabati,ananunua samani hakujua anapunguza mtaji wake?
bwana prondo nafikiri refurbishment ni sehemu ya mtaji, angefanyaje au hela ingekaa tu bila kufanya lolote..si bora naona kafanya jambo linaonekana ..je angeenda kuinywa bia au kuitumia kwenye starehe ingekuwaje
 
Si unaona kafanya ukarabati matokeo yake hela imeisha, angeingia hivyo hivyo kiugumuugumu au asingechukua fremu hadi mtaji ukue sana. Hujawahi kuona wale wanaofanya hio biashara ya tigopesa mpesa chini ya mwamvuli?

Vijana wengi wakiwa na ndoto za biashara wanapenda wawe na ofisi kubwa inavutia bila kujua hata future ya biashara yake. Matokeo yake anabaki kusifiwa tu ofisi nzuri sana huku imemlia mtaji wale mdogo matokeo yake kodi ikiisha baishara nayo kwisha.
 
Ila ukiona mtaji wako wa kuunga unga bora uwe kauzu utafute hata kibanda kuliko kulipa kodi
Au hata meza kwa Mpesa inafaa kabisa kuanzia.

Idea ni nzuri kama una namna unaweza kuweka share na mtu fanya hivyo
 
Ndio mimi nimemwambia angeanza chini ya mwamvuli hadi mtaji ukue.
 
Biashara ina muda gani? Maana kama eneo lina watu kama alivyosema sioni sababu ya msingi ya biashara kufa zaidi ya kuibiwa au kula mtaji.

Unataka kuniambia wateja wa M-Pesa na TigoPesa wameisha kiasi hicho?
.
Tatizo mi naonaga kwenye mahesabu ya kufungua biashara, hatuhesabu hela ya kujikimu wakati biashara haija changanya, matokeo yake mtaji huohuo ndo utoe hela ya kula.

Ndo hivyo yashatokea, ushauri wangu asifunge biashara, hizo ni changamoto za biashara wote tumepitia/tunapitia

Kama ni trustworthy na amejifunza mwenendo wa biashara. Afanye mpango wa kukopa kwa jamaa na marafiki. Na ahahikishe watu wake wa karibu wote wanampa kazi yeye ya Tigopesa na M-pesa. Atavuka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…