Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
Kuna haja ya kuwakaribisha Starlink Tanzania kwasababu zifuatazo
1: Starlink wanatoa huduma nzuri lakini ni ghali sana kulinganisha na makampuni yetu ya simu hapa Tanzania kwahiyo wao kuja haiwezi kuathiri au kuangusha huduma ya internet inayotolewa na makampuni ya simu
2: Wi-Fi ya Starlink haiwezi kuathiri makampuni ya simu kwasababu transmission yake sio ya minara kanakwamba Wananchi watapata huduma kwenye simu zao moja kwa moja pasipo kununua vifaa vya kunasa mawimbi ya internet
3: Ni ngumu sana wateja wa Wi-Fi za satellites kuhamia kwenye internet inayotolewa na makampuni ya simu au Wateja wa internet inatotolewa kupitia makampuni ya simu kuhamia Wi-Fi inayotolewa na Satellites namaanisha kwamba hapa kuna wateja wawili tofauti
Mfano rahisi ni kuwa watumiaji wa Apple ni tofauti na wa Android hivyobasi bidhaa za upande mmoja zinapokuja haziwezi kuathiri za upande mwingine kwahiyo hakuna haja ya kuzuia bidhaa za upande mmoja
4: Ukiachana na Starlink, hapa Tanzania kuna wateja wa Wi-Fi za Satellites tangu zamani sio kwamba ni jambo geni. Hivyobasi Starlink kuja hakuna anguko lolote kwa makampuni ya simu zaidi itachochea ushindani mkubwa kwa makampuni ya simu ili yazidi kuboresha huduma zake kwasababu hatua waliyofikia sasa bado haitoshi tunahitaji maboresho makubwa
5: Wi-Fi ya Satellites inawalenga wateja wenye kipato kikubwa kwahiyo mtu mwenye pesa nyingi huwa anatumia bidhaa za gharama kubwa kwahiyo apewe huduma anayotaka wala asinyimwe
6: Starlink kuingia Tanzania Serikali itaongeza mapato yake maradufu kulingana na makubaliano mtakayojiwekea
7: Kwenye swala la uchochezi au machafuko kwenye mitandao ya kijamii lishughulikiwe na kampuni za Social Networks kwasababu wao ndio wanaobeba maudhui ya watumiaji lakini sio watoa huduma ya internet
Kampuni ya Meta imeboresha sana huduma zake na huwa haiwavumilii watumiaji wanaoanzisha uchochezi au machafuko labda kama kuna kampuni nyingine ambayo inaruhusu maudhui hatarishi
Hivyobasi linapotokea swala la uchochezi katika mitandao ya kijamii, watumiaji walioanzisha washughulikiwe na wamiliki wa hiyo mitandao lakini kama wamiliki hao hawatawashughulikia ndipo Serikali iwawajibishe wamiliki wa hiyo mitandao kwa kosa la kukumbatia wahalifu