Ushauri kwa Mo juu ya overhaul

Huja

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2021
Posts
1,167
Reaction score
1,848
Mo...mmoja wa matajiri lialia wa simba kuwahi kutokea pale msimbazi.

Ni very rare kupata watu wa hivyo. Si mfadhili tu bali ni mshabiki anayeumia simba ikipoteza.

Yapo majungu juu yake ili akate tamaa, ila huyu jamaa watasubiri sana. Sio kama kina Azim Dewj wakati ule...the man is real ambitious. Tunajua umewekeza simba, leo timu inapata kila facilities..

Ni mwaka wa pili sasa Washabiki wanakosa lile shangwe na mzuka wa ''WAR IN DAR''.

Timu ipo CCL , 2nd NPL, inashinda lakini hakuna furaha..kwa nn? ...is like Barcelona kwamba hata washinde lakini kama hawachezi PIRA lao bado..

NINI KIFANYIKE.-

1: Unda timu makini ( ufundi) kwa ajili ya scout ya wachezaji hata kama sio maarufu but skilled, wepesi na wenye nguvu for CCL ( timu ya usajili for past 2 years imekuangusha sana )

2: Fanya scout ya kocha (mapema) badala ya zima moto ligi ikiisha (unless ROBERTINO abadilike lakini kwa jicho la mbali..mh mashaka..

3: Imarisha kitengo cha uhamasishaji, kuamsha Ari na mzuka kuanzia kambi ya team hadi kwa washabiki nchi mzima.

4: Tafuta watu wabunifu ndani ya SIMBA...

5: Anza kufikiria Mzabuni wa jezi anayejitambua .
6:.....
7:…..

Mo fanya mapinduzi makubwa ( OVERHAUL) ndani ya Simba. Yawezekana Mo uko busy sana for other Business management, investments and travelling... but Nasema haya kwa Mo kwa Kuwa una hisa kubwa ndani ya simba....una influence kubwa ktk decision making and strategies..

Uli-struggle - very hard to make transformations ndani ya SIMBA ..na ukafanikiwa kubadili mindsets za wazee na kuwekeza pale na kuleta walau usimamizi wa kisasa ktk vilabu vikubwa tz ( wengine wamekuja kuiga ideas zako za uthubutu).

Hatukujua ipo siku Simba itakuwa Top 11 club in Africa... Simba wanaalikwa kushiriki Africa super league for the first time.

Simba imetambulika kama Giant club in East and Central Africa ..

Let you be the champion of these football transformations ...
 
Tatizo Mo bahili na anapenda Sana janja janja ...hata deal ya Vunjabei inasemekana ni yeye anamtumia Vunjabei .. unafikiri ataweza fanya kazi na Nike au Adidas??
Jikite kwenye facts na sio hisia, kwani wenye jezi nzuri wote wame watumia Adidas au Nike ?

Nadhani mifano inajulikana wenye jenzi nzuri ...
 
Scouting ya Simba ipo hovyo sana. Yaani hata Singida na Azam wanawashnida kusajili wachezaji wazuri. Ukiangalia Simba ya Rebertihno kwa asilimia zaidi ya 80% ndio ile ile Simba ya Uchebe. Jiulize toka kaondoka Uchebe Simba imesajili wachezaji wasiopungua 6 kwa wastani kila msimu (dirisha kubwa na dogo) wameenda wapi ikiwa wanaocheza "first eleven" kwa kiasi kikubwa ni wale wale waliocheza miaka minne iliyopita wakati wa Uchebe?

Mfano mdogo usajilii wa dirisha dogo Simba iliwaongeza Sawadogo na Baleke lakini nao wameishia muda mwingi kwenye mbao ndefu.

Nini kifanyike?
Narudia tena kutoa mapendekezo yangu hapa kama nilivyofanya miaka miwili iliyoisha na uongozi wa Simba una hiyari kuyachukua kama wataona yanawafaa au waachane nayo kama wataona hayafai.
1. Kwanza waunde timu ya scouting yenye watu 10 kwa kutumia hazina ya wachezaji na makocha wa zamani walio na mapenzi ya dhati na Simba. Kwa kuanzia iwe kazi ya kujitolea kwa wale watakaokubali ila walipwe posho kila wanapokutana. Pesa itakayotumika kuwalipa posho na nauli itokane na kuondoka gharama za ovyo kabisa kama zile za kuwasha moto Afrika Kusini.
2.. Timu ya scouting ikae na benchi la ufundi na uongozi kuainisha maeneo yenye mapungufu kwenye timu pamoja na kuhakikisha kila nafasi uwanjani inakuwa na wachezaji wawili wanaoimudu vyema.
3. Baada ya kuainisha maeneo yenye mapungufu ndipo sasa uongozi uwasiliane na mawakala wa wachezaji na sio madalali wa wachezaji kwa nafasi na aina ya wachezaji wanaowahitaji. Na kwasasa Simba ni mojawapo ya timu kubwa Afrika kwa hiyo wanafahamu nani ni wakala na nani ni dalali. Zoezi hili lifanyike wakati ligi za nchi mbali mbali zinapoendelea badala ya mwishoni mwa msimu.
4. Baada ya kupata listi ya wachezaji wanaohitajika timu ya scouting kwa kugawanyika katika makundi ya watu watatu au wawili iwezeshwe kwa nauli na posho kwenda kuwaangalia hao wachezaji jinsi wanavyocheza kwenye ligi ya nchi zao na hata michezo ya kimataifa mara kwa mara ili kujiridhisha kuwa huyo mchezaji ana uwezo kweli. Pia kujua iwapo anacheza mara kwa mara au anakumbwa majeraha mara kwa mara.
5. Timu ya scouting ikisharidhika na uwezo wa mchezaji basi iushauri mapema uongozi ufuatilia mkataba wa mchezaji husika. Kuanzia hapo timu ya scouting itakuwa imemaliza kazi yake.
6. Kwa mlolongo huu Simba itakuwa inaokoa pesa nyingi sana kwa sababu sasa hivi inasajili wachezaji wa kimataifa kwa mamimilioni ya pesa kupitia kwa madalali na mawakala wasio makini halafu inawatoa kwa mkopo au inavunja mikataba nao kitu ambacho sio sahihi. Kwenye "youtube" kila mchezaji ni mzuri kwa sababu zinachukuliwa zile sehemu tu mchezaji alipofanya vizuri lakini ukiwa na timu ya scouting mchezaji anafuatiliwa kwa muda mrefu hata mwaka mzima kwa hiyo ni rahisi kujua uwezo wake halisi.

Angalizo
Usajili ni kama kamari. Unaweza kusajili mchezaji mzuri kabisa tena umemfanyia scouting na akaja kushindwa kukupa kile unachotazamia kutoka kwake na hata timu kubwa za ulaya hili limewahi kuwakuta. Lakini hii haimanishi kuwa scouting ya wachezaji isifanyike. Kikubwa scouting ifanyike kwa umakini na kwa muda mrefu angalau katika wachezaji 6 wanaosajiliwa akitokea mmoja au wawili wabovu sio mbaya kuliko sasa hivi unasajili wachezaji 6 tena wa kimataifa halafu wawili unawatoa kwa mkopo halafu 4 wanasugua benchi. Na mbaya zaidi hili jambo linajirudia kila msimu.

Ni mtizamo tu.
 
Soka la hii nchi huathiriwa na watu ambao hata huwajui mkuu.Mo si kama anashindwa mamlaka kamili ndo anakosa.Wanasiasa wapo kwenye soka, SHTUKA.
 
Natamani hii kitu ionekane na uongozi WA Simba!

Napendekeza Kitengo cha scouting apewe Boniphace Pawasa. Jamaa lugha anaijua haitamsumbua kutembelea nchi kadhaa na pia Mpira anaujua Kwasababu ana leseni ya Ukocha ukizingatia pia ni legend WA Simba.

Lakini Pia kwenye hiyo Scouting ya asikose Maestro Yule WA efm. Jamaa ndio kawatoa wakina mkude, Hajibu kama unakumbuka Ile Simba ya ukata .. Hawa vijana walikuwa Simba B chini yake Maestro.


Mkuu umeandika vizuri SAna.
 
Tatizo Mo bahili na anapenda Sana janja janja ...hata deal ya Vunjabei inasemekana ni yeye anamtumia Vunjabei .. unafikiri ataweza fanya kazi na Nike au Adidas??
Mkuu nike na adidas hawawez kuja fanya kazi na mapacha wa kariakoo kwa sasa, wao wapo na team kubwa, labda Umbro na Uhlsports

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Hanspope hanspope hanspope
 
Mo ni CHUPLI CHUPLI.

Huwa anaenda na Matukio.

Kuna wakati Huwa anajitoa, Kuna wakati Huwa anarudi.

Ana ingia TOKA INGIA TOKA nyinginsana.
GSM waliitaka Simba.
BAHARESA aliitka Simba nknk...

MO NDIO KIRUSI CHA SIMBA
 
Mwisho wa siku watu wanataka PESA ww unaleta story tu
 
Mimi nikiona tu mtu anaweka neno "inasemekana" ninaanza kuwa na wasiwasi na hoja yake kuliko hata hicho kinachosemekana
Kwa sbb hana uhakika basi na hoja yake ni batili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…